Msikiti wa Sogea uliopo jirani na Branchi ya Sogea unawaomba Waislamu popote mlipo katika ulimwengu huu wa Arrahmaan kuungana nao katika kukimaliza kisima cha maji kilichopo nje ya Msikiti ambacho kilianzwa kuchimbwa kwa juhudi za Waislamu ila wameishiwa nguvu na hivyo kuwaomba Waislamu Sadaka zao.
Kisima imebidi kiongezwe chengine baada ya kuzidiwa nguvu kwa kisima kilichopo sasa ambacho hakitoshelezi mahitaji ya maji kwa msikiti kutokana na wingi wa Waislamu wanaokufika msikitini kwa shughuli za Ibada.
Gharama iliyobakia kumalizia kisima hiki ni takriban Shilingi Milioni moja na Nusu tu.
Ndugu yangu Muislamu na katika Imani, jitahidi isikupite fursa hii adhimu na adimu ya kujiwekea akiba isiyooza au kuharibika huko tuendako kwa kutoa Sadaqatun Jaariyah (Sadaka yenye kuendelea)
Allaah Subhaanahu Wata'ala anatukumbusha katika Qur'aan "Na kheri yoyote mtakayoitanguliza kwa ajili yenu basi mtaikuta mbele ya Allaah itakuwa kheri kubwa na (yenye) ujira mkubwa" Suuratul Muzammil
Kwa maelezo zaidi na vipi kuwasilisha sadaka yako, wasiliana na Imaam wa Msikiti wa Sogea Sheikh Suleiman Bin Daaud +255 777 460 056
Sehemu ya eneo la kisima ambacho mbali na kutoa maji na kuhudumia Msikiti pia wakaazi wanaoishi maeneo ya karibu hutegemea kisima cha msikiti kwa kupata huduma hii iliyoadimika ya maji kwa kuchangia msikiti.
Msikiti wa Sogea ambao upo Barabarani na waumini wengi hufika kwa kusali Sala tano pamoja na Sala ya Ijumaa. Msikiti huwa unajaa wakati mwengine mpaka watu kukosa kusali
Sehemu ya kisima chenyewe ambacho kimefunikwa kwa sasa ili kisiharibike