Mfanyakazi wa Kampuni ya JAK, Bi.Aziza Khamis akitowa maelezo kuhusiana na matumizi ya vifaa vya uokoaji vinavyotumika katika boti zao zinazotowa huduma ya usafiri kwa abiria wanaotumia boti zao kati ya Unguja na Pemba.
Afisa wa Kampuni ya Azam Marine akitowa maelezo kuhusiana na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo, kwa wananchi waliofika katika maonesho ya Tamasha la Wadau wanaotowa huduma ya usafiri wa baharini.
Afisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)Ndg.Muhamad Masoud, akitowa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda lao katika maonesho ya Siku ya Usafiri wa Baharini Duniani yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Salama bwawani.
Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, Bi.Raya Hamad, akitowa huduma kwa mteja wake aliyefika katika banda lao kujuwa kiwango cha mchango wake aliojichangia katikla mfuko huo, wakati wa maonesho ya Tamasha la Siku ya Usafiri wa Baharini Duniani,yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi wa salama bwawani.
Afisa wa Mamlaka wa Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) akitowa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea maonesho hayo katika banda lao, kuona huduma zinazotolewa na Idara hiyo.
Afisa Uvuvi wa Idara ya Deep Sea Fishing Bi Mary Nkomola, akitowa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi wa salama bwawani.
Eng. Hassan Msumi, wa Chuo cha Bandari Tanzania akitowa ufafanizi na huduma zinazotolewa katika chuo hicho kwa wanafunzi wanaojiunga kusomea mambo ya bahari.
Captain Mahbuub akiwa katika banda lao la Kampuni ya Meli ya DANAOS SHIPPING Co. inayotowa huduma za mafunzo ya Ubaharia Zanzibar na ajira kwa Vijana wa Zanzibar.
Afisa wa Kikosi cha Wanamaji Zanzibar KMKM, Ndg. Hussein Ali Makame, akitowa maelezo kwa mwananchi aliofika katika banda lao kujionea huduma za uokoaji na uzamiaji kwa Askari wa kikosi hicho.
Afisa wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Marine Ndg.Twalib Masoud, akitowa maelezo ya matumizi ya mtambo wa kuchunguza minendo ya safari ya vyombo vya baharini kijilikanacho kwa jina Sea Vision, wakatin wa maonesho ya vyombo vya usafiri wa baharini.