Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hifadhi ya Msitu wa Jozani yaundiwa "Halmashauri ' Ili kukabiliana na Uharibifu wa MSITU HUO

$
0
0
Na Faki Mjaka- Maelezo.
Idara ya Misitu Zanzibar imeanzisha “Halmashauri ya Wanajamii wanaoizunguka Hifadhi ya Msitu wa Jonzani” ikiwa ni Mkakati wa kukabiliana na Uharibifu unaoendelea kufanywa katika Msitu huo.

Halimashauri hiyo inayowashirikisha Wanajamii itakuwa na jukumu la kukutana kila Mwezi kujadili changamoto na Mafanikio yanayopatikana katika kutunza Msitu huo wa Taifa.

Akizungumza mara baada ya Kuanzishwa Halimashauri hiyo Afisa kutoka kitengo cha Misitu ya Serikali Ally Mwinyi amesema wameamua kuanzisha Halmashauri kutokana na kuendelea kukithiri kwa Vitendo vinavyohujumu Msitu huo ambao ndio tegemeo kwa maendele ya Zanzibar.

Amesema licha ya kuundwa kwa Bodi ya Hifadhi ya Jonzani Ghuba ya Chwaka bado kuna Vijiji ambavyo vinazidi kuhusika katika kuuharibu Msitu huo jambo lililopelekea kuanzishwa kwa Halimashauri hiyo ambapo Wananchi watakuwa wakihusishwa mojakwa moja katika maamuzi ya kusimamia Uhifadhi wake.

“Kuundwa kwa Halmashauri hii kutatoa fursa kwa Wanavijiji wao binafsi kubeba jukumu la kuuhifadhi  Msitu na kutoa elimu miongoni mwao badala ya jukumu hilo kufanywa kwa kiasi kikubwa na Bodi ya Uhifadhi” Alibainisha Mwinyi
Kwa upande wake Mwenyekiti aliyechaguliwa na Halmashauri hiyo Mwalimu Aziz Abdallah Vuai amesema atahakikisha anatumia muda wake mwingi ili kutoa Elimu kwa jamii juu ya matumizi ya Nishati mbadala kwa ajili ya kupikia.


Amefahamisha kuwa Wanavijiji wengi wamekuwa wakihujumu Msitu huo kwa kukata Miti kwa ajili kutengeneza Mkaa na Kuni za kupikia na hivyo njia pekee ya kuepuka tatizo hilo ni elimu ya kutumia Nishati mbadala ya kupikia.

Aidha ameongeza kuwa atawashajihisha Wakulima katika Vijiji Jirani na JONZANI kutumia kilimo cha Umwagiliaji ili kisaidie katika kukabiliana na mahitaji yao badala ya kuingia katika Msitu huo kwa lengo la kufanya shughuli za kilimo.

Halimashauri hiyo iliyoundwa itakuwa ikikutana kila Wiki ya Mwisho ya Mwezi ambapo wajumbe wawili kutoka Shehia tisa zinazozunguka Hifadhi ya Msitu wa Jonzani ikiwemo Chwaka, Cheju, Unguja Ukuu, Pete, Kitogani, Bwejuu, Michanvi na Charawe zitapata fursa ya kupanga mikakati ya kuuhifadhi Msitu huo.

Hifadhi ya Msitu wa Jonzani ni miongoni mwa Vivutio vikubwa vya Utalii ambapo pamoja na faida nyingine Hifadhi hiyo imesaidia kupatikana kwa Umeme wa Uhakika, Maji na Ujenzi wa Skuli katika Vijiji jirani ya Hifadhi hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>