Na.Khadija khamis na Rahma Khamis ZJMMC..
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya maji Zanziabar ( ZAWA) Zahor Sleiman Khatib amesema bado kuna changamoto nyingi zinazoikabili Taasisi hiyo ikiwemo upungufu wa visima katika baadhi ya maeneo ya vijijini .
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisisni kwake, alisema kuwa Mamlaka ya Maji inaendelea kuwapatia huduma wananchi wa Zanzibar na kuwahamasisha wananchi wa maeneo ambayo bado hawana uwelewa wa kuchangia huduma hiyo ili waweze kuchangia.
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuchangia asilimia 11 mpaka 21 kwa matumizi ya majumbani, na asilimia 80 kwa wafanyabiashara hasa mahotelini.
“Bado tunahitaji nguvu ya pamoja kuiendesha vizuri huduma ya maji safi kwa sasa mapato tunayokusanya hayakidhi kuendeshea huduma”. alisema Zahor.
Alisema kuwa changamoto ambazo wanakabiliana nazo kwa sasa ni tabia ya baadhi ya wananchi kukataa kuchimbiwa visima katika maeneo yao kama ilivyotokea Bumbwini makoba .
Akizungumzia mifereji ambayo ZAWA waliitoa katika baaadhi ya maeneo ni kutokana na kukosa udhibiti na uangalifu wa mifereji hiyo.
Alisema kuwa katika zoezi la kuifunga mifereji ambayo ilikosa washungulikiaji wananchi walijikusanya na kuandaa utaratibu wa kuidhibiti hasa katika vijiji vya Jambiani, Makunduchi na Muyuni.
Ndugu Zahor amesema huduma ya maji safi na salama kwa wananchi inatarajiwa kufikia asilimia 90 kuanzia mwakani baada ya juhudi kubwa ya kuchimba visima vipya kwa msaada wa wafadhili wa Bank ya maendeleo ya Afrika (ADB ) na Rasul hema .
Afisa uhusiano wa ZAWA aliwashauri wananchi kutumia maji kwa uangalifu mkubwa kwani kila tone moja ni gharama .