Na Zainab Anuwar
Mkurugenzi wa Manispaa Zanzibar, Abedi Juma Ali, wamewataka wafanyabiashara wa soko la kuku Darajani kufanya shughulia katika hali ya usafi.
Aliyasema hayo wakati akizindua kifaa cha kuchujia manyoa ya kuku kwa lengo la kuweza kudhibiti utapakaaji wa manyoa hayo ndani na nje ya soko hilo.
Alisema kifaa hicho kitasaidia kiwango kiasi kikubwa kulinda mazingira katika soko hilo.
Aidha aliwataka kushirikiana na manispaa kuhakikisha hali ya usafi inaimarishwa katika soko hilo.
Mwenyekiti wa Glitters Volunteer Group Zanzibar Cleaning, Mohamed Khamis, alisema manyoa ni mali ambayo hutumika kutengenezea mambo mbali mbali kama vile nguo pamoja na kutumika kama ni mbolea.
Hata hivyo, alisema bado soko la manyoa kwa Zanzibar ni dogo kutokana na idadi ndogo ya kuku wanaochinjwa.
Alisema kifaa hicho kitasaidia kutunza mazingira ya soko hilo na utapakaaji wa manyoya uliozoeleka katika soko hilo.