Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Ali Iddi, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA Chuo Kikuu Huria Tawi la Zanzibar, huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanziabr.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Prof. Tolly Mbwette akimpa maelezo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Ali Iddi, kuhusu shughuli za mafunzo wanayoendeshwa chuoni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma chuo Kikuu Huria Kituo cha Zanzibar wakiwa kwenye chumba cha Komputa .
Mkurugenzi wa Kituo cha Uratibu cha Zanzibar cha Chuo kikuu huria cha Tanzania Yusuph Mussa akitoa maelezo mafupi ya Kituo hicho, , huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanziabr
Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi baada ya uzinduzi wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA kwenye kituo cha Uratibu cha Zanzibar huko Beit el ras nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Prof. Tolly Mbwette akimpa maelezo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Ali Iddi, kuhusu shughuli za mafunzo wanayoendeshwa chuoni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma chuo Kikuu Huria Kituo cha Zanzibar wakiwa kwenye chumba cha Komputa .
Mkurugenzi wa Kituo cha Uratibu cha Zanzibar cha Chuo kikuu huria cha Tanzania Yusuph Mussa akitoa maelezo mafupi ya Kituo hicho, , huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanziabr
Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi baada ya uzinduzi wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA kwenye kituo cha Uratibu cha Zanzibar huko Beit el ras nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wahaziri na Wakurugenzi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmin mara baada ya uzinduzi wa maabara ya mafunzo ya TEHAMA Chuo Kikuu Huria Tawi la Zanzibar, huko Beit rasi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar).
Na Khadija Khamis na Miza Othman –Melezo Zanzibar
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali IDDI amewata wananchi kutumia fursa iliyotolea na Chuo Kikuu Huria Tanzania kujiendeleza zaidi kwa mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho kwani kutawajengea uwezo wa kupata taaluma, maarifa, utambuzi pamoja na kuchanganuwa masuala mbali mbali yatakayosaidia katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo
Ameyaeleza hayo alipokuwa akizinduwa Maabara ya Mafunzo ya TEHAMA katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kituo cha Uratibu cha Zanzibar kilichopo Beit el ras.
Balozi Seif amewataka wananchi kutumia fursa ya kujifunza masomo ya TEHAMA kutokana umuhimu wake hasa wakati huu wa mabadiliko makubwa ya Sayanasi na Teknolojia duniani.
Amesema Serikali hivi sasa inaendelea na ujenzi wa mkongo wa Taifa ambao lengo lake ni kuunganisha Wilaya zote Zanzibar na pia kuunganishwa na mtandao wa kimataifa ambao huunganisha nchi zote ulimwenguni.
“Bila shaka wengi wetu tumeshasikia kuhusu Mkongo wa Taifa wa mawasiliano kwa kutumia kompyuta ambayo ujenzi wake unaendelea nchini kote”, alisema Balozi Seif Ali Idd.
Ameongeza kuwa zoezi hilo litakapo kamilika thamani na manufaa ya Mkongo wa Taifa yataonekana endapo wananchi watakuwa na ujuzi wa kutumia TEHEMA.
Balozi Seif aliupongeza uongozi wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania kwa kasi kubwa ya maendeleo inayopiga katika kusambaza elimu kwa watanzania.
“Elimu ndio silaha kubwa katika masisha hivyo juhudi hizi ni za kulindwa, kupongezwa na kujengewa mazingira mazuri ya kuboreshwa kila inapohitajika badala ya kuzibeza kwa sababu wanaofaidika ni Wazanzibari,”alisisitiza balozi Seif Ali Iddi.
Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Tollys. A. Mbwette amesema ni vyema wafanyakazi kutumia fursa ya huduma za Chuo hicho kwa kujiendeleza ili waweze kunufaika na mafunzo yanayotolewa ambayo yatawasaidia katika kurahisisha utekelezaji wa kazi pamoja na kuongeza ufanisi.
Amesema lengo la kuanzisha kwa mafunzo ya TEHAMA hapa Zanzibar ni kuwasaidia wananchi kwenda sambamba na ukuaji wa matumizi ya Sayansi na Teknolojia.
“Mafunzo haya ya matumizi ya TEHAMA yatakayotolewa na Kituo cha Uratibu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yamelenga katika kuwahamasisha watu mbali mbali waliopo Zanzibar ili kupata maendeleo ya haraka katika matumizi ya Teknolojia,” alisema Makamu Mkuu wa Chuo.
Chuo cha Kikuu Huria cha Tanzania kimeanzishwa mnamo mwaka 1993 hadi oktoba 2012 jumla ya wahitimu 14,288 ambao kati yao 6075 wamehitimu vyeti na stashahada , 6655 Shahada ya kwanza 1558 walihitimu masomo ya Uzamili, Uzamivu na Shahada za udaktari za heshima.