Waandishi na maafisa habari wa nchi mbali mbali wakitembelea majengo ya kihistoria katika miji ya Agra na Jaipur, Kaskazini mwa India. Mbele kulia ni mwandishi Hassan Hamad wa (OMKR). (Picha zote kwa hisani ya Hassan Hamad, India).
Muongozaji watalii, akitoa maelezo kwa waandishi na maafisa habari wa nchi mbali mbali waliotembelea majengo ya kihistoria katika miji ya Agra na Jaipur, Kaskazini mwa India. Katikati ni mwandishi Hassan Hamad wa (OMKR).
Muongozaji watalii, akitoa maelezo kwa waandishi na maafisa habari wa nchi mbali mbali waliotembelea majengo ya kihistoria katika miji ya Agra na Jaipur, Kaskazini mwa India. Wa pili kulia ni mwandishi Hassan Hamad wa (OMKR).
Waandishi na maafisa habari kutoka baadhi ya nchi za Afrika, Asia na Latin America wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la kihistoria la Taj Mahal nchini India, wakati wakiwa katika ziara ya kimasomo. Taj Mahal ilijengwa na mtawala Shah Jahan wa India katika karne ya 17 kama kumbukumbu ya mke wake mpendwa aliyefariki kabla yake aliyejulikana kwa jina la Mumtaz Mahal. Likiwa na wafanyakazi wa ujenzi 22,000 ilichukua miaka 22 hadi kukamilika kwake.