Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Zitto atunukiwa tuzo ya mtetezi wa haki ya hifadhi ya jamii

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, ameibuka mwanasiasa wa kwanza barani Afrika kutwaa tuzo ya mtetezi wa haki ya hifadhi ya jamii, imefahamika.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), Zitto anatarajiwa kukabidhiwa tuzo yake hiyo katika sherehe rasmi iliyopangwa kufanyika Oktoba 30 na 31 mwaka huu katika mji wa Livingstone nchini Zambia.

“Tuzo hii imetolewa kwako kwa kuzingatia mchango wako mkubwa unaoutoa kuhakikisha sehemu kubwa ya Watanzania ambao walikuwa hawanufaiki na mifuko hii wanafaidika nayo,” ilisema taairifa hiyo.

“ECASSA, mahususi kabisa, imevutiwa na jitihada zako za kuhakikisha kwamba wasanii wananufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na wakulima kupitia chama chao cha ushirika cha Rumako kilichopo Kigoma Vijijini,” iliongeza sehemu ya barua ya umoja huo kwa Zitto.


RUMAKO ni Ushirika wa Msingi wa Vijiji vya Mkabogo, Rusaba na Matyazo wilayani Kigoma Vijijini ambako zaidi ya wakulima wake 750 wameingia kuwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kwa takribani miaka minne sasa, Zitto amekuwa akipigania wakulima wa Tanzania kupewa uanachama wa wa mifuko hiyo ili kuwakwamua kiuchumi na pia kuwawezesha kupata huduma ya hifadhi kama ilivyo kwa wafanyakazi katika sekta rasmi wanaopata huduma hizo.

Akizungumzia tuzo hiyo, Zitto alisema, "Nimeipokea tuzo hii kwa unyenyekevu mkubwa. Naamini kuwa siku za usoni haki ya hifadhi ya jamii kwa wananchi itakuwa ni haki ya kikatiba.”

Alisema nchi masikini zinapaswa kuongeza uwekaji akiba ili ziweze kuendelea kwa kasi kwani bila akiba uwekezaji unakuwa mdogo na hatimaye uchumi haukui.


ECASSA ni umoja unaounganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii takribani 20 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Zambia.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>