Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Viongozi wanaojilimbikizia mali kitanzini

$
0
0
Na Mwantanga Ame
MSWADA wa sheria itakayowabana viongozi wa umma watakaokiuka maadili, unatarajiwa kuwasilishwa katika kikao kijacho cha Baraza la Wawakilishi, imefahamika.

Sheria hiyo itaanzisha Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambapo pamoja na kazi nyengine, itakuwa na mamlaka ya kuwabana viongozi wa umma kuhakikisha wanasalimisha mali zao.

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Oktoba 22 mwaka huu, ambapo Baraza la Wawakilishi limewataka wananchi kuuchangia kabla ya kuwasilishwa kwa wajumbe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Baraza la Wawakilishi na kuthibitishwa na Ofisa Uhusiano wa Baraza hilo, Himidi Choko, serikali imeamua kuwasilisha mswada huo ambao utasimamia maadili ya viongozi wote watakaotajwa kwenye jadweli la mswada huo.


Sheria hiyo itampa mamlaka Mwenyekiti wa Tume kumtaka kiongozi wa umma kuwasilisha kwake tamko la maandishi kuhusu mali anazomiliki.

Mbali ya mali zake, pia kiongozi atalazimishwa kutaja mali zinazomilikiwa na wakala wake, madeni anayodaiwa pamoja na mali na madeni ya mke au mumewe,watoto wao au watoto walio chini ya uangalizi wao.

Aidha Tume itakuwa na uwezo wa kupokea tuhuma na taarifa za uvunjwaji wa maadili kutoka kwa wananchi kwa kiongozi yoyote wa umma, kufanya uchunguzi juu ya madai au tuhuma hizo.

Mswaada mwengine ambao utawasilishwa unahusu mswada wa sheria ya kufuta sheria ya Wauguzi na Wakunga (Uanzishwaji wa Baraza la Usajili wa Wauguzi na Wakunga) Nam. 9 ya mwaka 1986, na kuanzisha badala yake sheria mpya ya wauguzi na wakunga na mambo yanayohusiana na hayo.

Mswada huo unaanzisha Baraza la Wakunga litakalokuwa na wajibu ya kusimamia fani ya wauguzi na wakunga.


Wananchi wametakiwa kuihangia miswada hiyo ambapo tarehe ya mwisho ya kupokea maoni ni Oktoba 12 mwaka huu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>