Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, amemteua, Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peter Ilomo, imesema uteuzi huo umeanza Ijumaa ya Oktoba 3, mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.
Mganga anachukua nafasi ya Dk.Eliezer Feleshi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo.