Muwezeshaji kutoka TASAF Pemba, Suleiman Ali Said akizungumza na wananchi walengwa wa shehia ya Ndagoni wilaya ya Chakechake Pemba, kwenye mkutano maalumu wa kuitambulisha miradi ya kuwapatia ajirza za muda walengwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa matuta ya kinga maji na barabara kwa hatua za kifusi
Wananchi walengwa wa shehia ya Junguni Jimbo la Gando wilaya ya Wete kwenye TASAF (III), wakimsikiliza mtaalamu juu ya namna ya kufanikisha ujenzi wa mtuta ya kinga maji, kwenye mradi wa kutoa ajira za muda kwao, ambapo mkutano huo uliofanyika skuli ya Junguni ulikuwa na lengo la kukusanya maoni yao kabla ya kutekeleza mradi huo
Msimamizi mkaazi wa kiwanda cha kuzalisha mpira Maziwani wilaya ya wete Pemba nd Saleh Suleiman Massoud kilicho chini ya kampuni ya Agro Tex Ltd, akiwaonyesha maofisa wa TASAF ambao walisimamisha msafara wao, kuangalia jinsi uzalishaji wa mpira, wakati maofisa hao wakiwa na ziara ya kuwakagua walengwa kwenye matayarisho ya miradi ya kutoa ajira za muda shehia za Junguni na Ukunjwi wilaya ya Wete Pemba,
Mpira ambayo tayari imeshakauka ikisubiri kufungwa pamoja kwa ajili ya kuisafirisha nje ya nchi kama vile Dubai kwa ajili ya mauzo, ambapo mpira huo unazalishwa eneo la Maziwani wilaya ya wete kisiwani Pemba na kampuni ya Agro Tax LTD.
Msimamizi mkaazi wa kiwanda cha kuzalisha mpira Maziwani wilaya ya wete Pemba nd Saleh Suleiman Massoud, akiwaonyesha maofisa wa TASAF ambao walisimamisha msafara wao kuangalia jinsi uzalishaji wa mpira kutoka kwenye miti wake, wakati maofisa hao wakiwa na ziara ya kuzikagua kaya kwenye kwenye matayarisho ya miradi ya kutoa ajira za muda shehia za Junguni na Ukunjwi wilaya ya Wete.