Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Siku ya mtoto wa kike kuadhimishwa Tarime

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali, leo kitaadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani kwa kufanya mjadala mpana juu ya kukomesha ndoa za utotoni nchini.

Mjadala huo utakaofanyika hoteli ya CMG-Motel mjini Tarime mkoani Mara na kufuatiwa na kilele chake tarehe kesho ni mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kutokomeza ndoa za utotoni ijulikanayo kama “Ndoa za umri mdogo, Ukanda Huru” iliyozinduliwa mwaka huu ikiwa na lengo la kuimarisha mienendo ya Taifa kwa ajili ya kuhakikisha viongozi wanawajibika katika kukomesha ndoa hizo kwa kuweka mikakati ili wasichana wapate haki zao.


Mwaka 2011, Baraza Kuu la Umoja wa Mataia lilipitisha maadhimio ya kuanzisha siku ya mtoto wa kike duniani. Siku hiyo imetengwa kwa ajili ya kuendeleza,kukuza haki na kutatua matatizo yanayowakumba wasichana. Kauli mbiu mwaka huu ‘Kuwawezesha Wasichana: Kumaliza Mduara wa Ukatili’ ambayo inatoa wito kwa wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa kuwekeza, kuwawezesha na kutokomeza aina zote za ukatili zinazowapata wasichana ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni.

Ndoa za utotoni ni suala linalohusu haki za binadamu; linakiuka haki za binadamu na kuzuia maendeleo kwa wasichana na wanawake.

Aidha Tanzania pekee, wastani wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 wakati  katika bara la Afrika zaidi ya asilimia 42  ya watoto wa kike wanaolewa kabla ya kufikia umri huo huku mamilioni wakiolewa wakiwa bado hawajafikia umri wa kubalehe.

Vile vile nchi 31 kati ya 41 duniani ambapo mwenendo wa kuozesha watoto wa kike unakaribia asilimia 30 zimo Afrika.

Katika miaka ya nyuma na hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mahitaji makubwa kwa serikali na mashirika mbali mbali duniani kutaka kutatua tatizo la mimba za umri mdogo  kama vile kutolewa kwa Mkataba wa Kutokomeza aina zote za Ukatili dhidi ya Wanawake (CEDAW) na Itifaki ya Maputo ambayo inakataza ndoa za utotoni.


Hivyo ahadi, maazimio na mikataba hiyo inapaswa ifanyiwe kazi kwa vitendo ili kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya wasichana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>