Na Kija Elias, Moshi
MKAZI mmoja wa eneo la Sabuko kata ya Ibiriri wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu,na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita, amethibitisha kutokea tukio hilo na kumtaja mtuhumiwa kuwa ni Emmanuelo John, ambaye ni mjomba wa mtoto huyo.
Alisema mtuhumiwa anadaiwa kufanyatukio hilo Oktoba 8, mwaka huu majira ya saa 10:45 jioni katika eneo la Sabuko kata ya Ibiriri, wilayani Siha mkoani hapa.
Alisema mama mzazi wa mtoto huyo alimwacha mtoto wake nyumbani na mjomba wake huyo, huku yeye akienda kujitafutia riziki na ndipo aliporejea alikumta mtoto huyo akiwa analia huku akitokwa na damu sehemu za siri.
Alisema mtoto huyo kwa sasa anapatiwa matibabu hspitali ya taifa ya Kibong’oto na kwamba mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa.
Alisema matukio ya ubakaji kwa sasa yameendelea kuongezeka mkoani Kilimanjaro na hivyo, kuwataka wazazi kuwa makini na watoto wao.