Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akitowa Mada katika Kongamalo la kuzungumzia Katiba Mpya ya Tanzania baada ya kupitishwa na Bunge Maalum la Katiba lililom,alizia kazi hiyo wiki iliopita, akisoma baadhi ya Vifungu vilivyopitishwa na Bunge hilo. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserekali ya Tanzania Yuoth Icon (TAYI) lililowakutanisha Vijana mbalimbali katika ukumbi wa Ekrotanali.
Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Kongamano hilo la Vijana kuzungumzia Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano iliopitishwa na Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
Vijana wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Ekrotanali Zanzibar.
Kijana Mtaalam wa Lugha za Ishara katika Kongamano hilo akitowa ishara ya mazungumzo kwa Vijana wenye ulemavu wa kutokusikia walioshiriki katika Kongamano hilo katika ukumbi wa Ekrotanali.
Baadhi ya Vijana wanaoshiriki Kongamano la Vijana kuzungumzia Katiba Mpya ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserekali ya TAYI na kuwakutanisha Vijana mbalimbali kuzungumzia Katiba. Kutoa elimu ya kuifahamu Katiba hiyo
Vijana wakichagia na kutaka kujuwa baadhi ya Vifungu vya Katiba kutoka kwa Aliyekuwa Mbunge wa Bunge Maal;um la Katiba na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni, alipokuwa akisoma baadhi ya vifungu hivyo katika Kongamano hilo.
Vijana walikuwa na hamu ya kujuwa na kutaka ufafanuzi kwa baadhi ya vifungu vya Katiba ilioyopendekezwa na Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, lililomaliza kazi hiyo wiki iliopita mjini dodoma.