Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mbunge wa Kikwajuni Atembelea Mradi wa Maji Jimboni

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni ametowa changamoto kwa Wanasiasa kutatua matatizo ya Wananchi kwa vitendo badala ya kutumia matatizo hayo na kero zao kwa  kujinufaisha wao.

Amesema hayo wakati wa ziara yake kutembelea mradi mkubwa  wa maji safi na salama kwa Wananchi wa jimbo lake, baada ya kukamilika kwa Mradi huo awamu ya kwanza ya uchimbaji wa kisima huko maeneo ya kaburi kikombe na kutandaza mabpmba ya maji.

Mhe Masauni amesema mafanikio ya Mradi huo na miradi mengine katika jimbo lake yametokana na nguvu za Wananchi kwa kutaka maendeleo katika jimbo lao la kikwajuni yanayotokana na misaada na mashirikiano makubwa kati ya wadau wa maendeleo wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Amesema mradi huo mkubwa wa maji safi na salama uko katika hatua ya mwisho kwa kuweka miundombuni ya kusambaza maji, ya utandazaji wa mabomba ya maji kwa sasa tayari utandazaji wa mabomba hayo yameshafika katika hatua kubwa kwa kutandika eneo kubwa na kufikia katika hutua ya kuunganisha na tangi lililoko mnara wa mbao kilimani.


Ufungaji wa Tangi jipya unatarajiwa kukamilika si muda mrefu na ili kuhifadhia maji hayo na kusambaza kwa wananchi wa jimbo la Kikwajuni na maeneo jirani. amesema tangi hilo lina uwezo wa kuhifadhi lita nyingi za maji na kuondoa tatizo la maji katika jimbo lake.

Pia amewataka Wananchi kuunga mkono Katiba Mpya iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba lililomaliza kazi yake hivi karibuni na kukabidhi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete na Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Dodoma. 



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>