Na Madina Issa
Idara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar, imesema mtoto aliyetupwa katika pwani ya Mawe matatu maeneo ya Migombani, anaendelea vizuri na kwa sasa yupo nyumba ya kulelea watoto Mazizini.
Akizungumza na Zanzibar Leo, Mkurugenzi wa idara hiyo, Halima Maulid Salum, alisema utaratibu wa idara ni kukaa na mtoto kwa muda wa mwezi mmoja na kama atatokea mtu anaeaminika akamtaka apewa.
Alisema tayari wameshajitokeza watu wengi kumuomba mtoto huyo lakini idara inaendelea kuwachunguza ili mmoja
atakaekubalika apatiwe mtoto huyo kwa ajili ya kumlea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema mtoto huyo kwa sasa yupo chini ya mikono salalama ya idara ya ustawi wa jamii.
Hata hivyo, alisema polisi wanaendelea kumsaka mtu aliyemtupa mtoto huyo.
Mtoto huyo alitumwa akiwa kwenya fuko la uzazi, tukio lililotokea Septemba 24 mwaka huu saa 11:00 jioni.