Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ufunguzi wa Mkutano wa Majiji na Manispaa Jijini Mwanza.

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndg.Zuberi M.Samataba, akifungua Mkutano wa Halmashauri za Majiji na Manispaa kutunza na kuhifadhi miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao. unaofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ndg.Onour Ozly, akizungumza katika mkutano huo wa Watendaji wa Majiji na Manispaa uliofanyika Mjini Mwanza na kuwashirikisha Maofisa wa Taasisi hizo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli yaGold Crest Jijini Mwanza
Mwakilishi wa Danida Tanzania Bi Jane Jacob. akitowa salamu za Taasisi yake wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Mji Mwanzawakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank) DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP).unaofanyika katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza
Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Majiji na Manispaa wakipongeza jambo lililowakilishwa katika mkutano huo wa Maofisa Watendaji. 
Mhandisi Ndg. Ezekiel Magoti, akitowa mada katika mkutano wa Halmashauri za Majiji na Manispaa kutunza na kuhifadhi miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao. unaofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.

Na: Atley Kuni- Afisa habari  Mwanza.
Halmashauri za majiji na manispaa zimehimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.
Kauli hiyo imetolewa mapena hivi leo na Zuberi Samataba, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza wakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank) DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP).
Samataba, amesema, kuna haja kwa kila halmashauri kuhakikisha inatunza miradi yote ambayo inafadhiliwa na wahisani hata baada ya wahisani kumaliza muda wao na kuondoka  kasha  miradi hiyo mikononi mwa Halmashauri. "Nivema mkawa  mnatenga fedha kwa ajili yakuhudumia miradi inayo anzishwa na wafadhili kwa ajili ya ukarabati na kuimarisha  ili iendelee kudumu kwa muda mrefu hata baada ya miradi hiyo kuisha muda wake na wafadhili kuicha mikononi mwetu".
Katika hatua nyingine  amewaagiza watendaji hao kutoa taarifa kwa wakati ili kujenga imani kwa wafadhili wanao toa fedha zao kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo wanayo ifadhili, "Wenzetu suala la mrejesho ni muhimu sana lakini zaidi sana mrejesho kwa wakati,  kwani  ni kama wanasheria wanavyo amini kuwa HAKI ILIYO CHELEWESHWA NI HAKI ILIYO NYIMWA". kwa mantiki hiyo kutoa taarifa kwa wakati ni suala muhimu sana,  vinginevyo au kinyume chake nikuwafanya wafadhili kupoteza imani kwa wanao wafadhili kwenye miradi amesema na kuongeza kuwa kwakuwa serikaliinaondoka kwenye utendaji wa kawaida na kuelekea kwenye utendaji wa upimaji ufanisi kwa matokeo (Performance for Result ) hivyo moja ya kigezo muhimu kitakachotumika ni kupima matokeo ni uwasilishaji wa taarifa kwa wakati.
Kikao hicho cha siku tatu kina wakutanisha Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Halmashauri Jiji la Mwanza , Manispaa ya Ilemela, Manispaaya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Dodoma, (CDA), Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Halmashauri ya mikindani Mtwara, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha pamoja na wawakilishi wa DANIDA sambamba na  World Bank.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>