Mchezaji wa timu ya Mofunzo Said Mussa akiondoa mpira galini kwake wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya grand malr, uliofanyika uwanja wa amaan, timu ya Mafunzo imeshinda 1--0.
Benchi la ufundi linapokuwa chgungu kwa makocha inawalazimu kutumia muda mwingi kusimama kufuatilia mchezo huo, kati ya timu yake na Mafunzo ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu kuchaguliwa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo baada ya kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Ali Bushiri kuenguliwa katika nafasi ya kocha mkuu na kuwa kocha namba tatu.
Mchezaji wa timu ya Mafunzo Ali Juma kushoto akijaribu kuwapita wachezaji wa timu ya KMKM Juma Mbwaba(8) wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Mafunzo imeshinda 1--0
Mshambuliaji wa timu ya KMKM akiwapita mabeki wa timu ya Mafunzo katika mchezo wao wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan.timu ya mafunzo imeshinda 1--0.
Mshambuliaji wa timu ya KMKM Maulid Ibrahim kapenta akiruka juu kupiga kichwa mpira huku beki wa timu ya Mafunzo Kheri Salum, akijiandaa kumzuiya katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan.
Kocha Mkuu wa timu ya KMKM Shaban Ramadhani akiwafokea wachezaji weake wakifanya vibaya uwanja wakati wa mchezo wa ligi kuu ya grand malt uliofanyika uwanja wa amaan.Kocha Shabani amechukuwa nafasi ya Kocha Ali Bushiri kuenguliwa nafasi hiyo hivi karibuni.
Kizaazaa golini kwa timu ya Mafunzo wakicheji wa timu ya KMKM wakiruka kuwania mpira.Beki wa timu ya Mafunzoo Haji Abdi akiondoa mpira galini kwake huku mchezaji wa timu ya KMKM Juma Mbwana, akimfuatilia katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan.
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya KMKM Ali Bushiri akiwa jukwaa la VIP akifuatilia mchezo wa ligi kuu kati ya timu yake ya zamani KMKM na Mafunzo akiwa na Kocha Juma wakizungumza huku mchezo ukiendelea katika uwanja wa amaan, timu ya KMKM imefungwa bao 1--0.
Kocha Mkuu wa timu ya KMKM Shaban Ramadhan, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na timu yake kukubali kipigo cha bao 1--0 dhidi ya timu yake ya zamani ambayo amewahi kuifundisha na kuchukuwa Ubingwa wa Zanzibar.