Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Bilioni 1.4 kutumika kukamilisha zoezi la usajili wa ardhi

$
0
0
 Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE 2.
  Afisa Mtambuzi na Msajili wa Ardhi Shawana Sudi Khamis kulia akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari hawapo pichani, katikati ni Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi na kushoto ni Mshauri wa Kiufundi wa zoezi hilo Andrew Smith. Mkutano huo ulifanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE.
Baadhi ya Waandishi wa habari waliokuwepo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar Wakimsikiliza Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi(hayupo pichani) kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE 2. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo ZANZIBAR

Na Amina Abeid-ZJMMC 22/08/2013
 
Jumla ya Shilingi Bilion 1.4 za Kitanzania zinatarajiwa kutumika kukamilisha zoezi la Kitaifa la Utambuzi na Usajili wa Ardhi ambalo limeanza rasmi katika Visiwa vya Unguja na Pemba.
 
Zoezi hilo linagharamiwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Finland iliyochangia Shl. Bilion 1 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyochangia Million 400 chini ya Mradi wa Usimamizi endelevu wa Ardhi na Mazingira Awamu ya Pili (SMOLE 11)
 
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Kikwajuni Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar  Januari Fusi amesema Usajili wa Ardhi hauhitaji malipo yoyote bali kinachohitajika ni Vielelezo muhimu katika zoezi hilo.
 
Amevitaja vielelezo hivyo kuwa ni Kitambusho cha Mzanzibari au Pasi ya kusafiria pamoja na Cheti cha kuzaliwa kwa Mmiliki wa eneo linalohitaji kutambuliwa kisheria.
 
Amefahamisha kuwa Mradi wa Smole 2 ulikuwa ni Mradi wa Miaka 4 ulioanza Mwaka 2010 na kutegemewa kumalizika mwaka 2013 lakini kutokana na kutokukamilika Serikali ya Zanzibar na Finland zimekubaliana kuongeza mwaka mmoja hadi Disemba 2014.
 

Amesema lengo kuu la kuongeza mwaka ni kuhakikisha Utambuzi na Usajili wa Ardhi katika maeneo yote unafanyika ili kuondoa migogoro ya Ardhi iliyodumu kwa muda mrefu Zanzibar.
 
Ameongeza kuwa Zoezi hilo litaongozwa na Ofisi mbili zilizopo chini ya Idara ya Ardhi na Usajili ambazo ni Ofisi za utambuzi wa Ardhi Unguja na Pemba na Ofisi ya Mrajisi wa Ardhi Zanzibar.
 
Ameyataja maeneo ambayo zoezi la Utambuzi limeanza kuwa ni pamoja na Nungwi, Jendele, kwa Ali Nathoo na Paje kwa upande wa Unguja ambapo kwa Pemba zoezi hili litaanza kwa Shehia za Selem, Wara na Uweleni.
 
Kwa upende wake Afisa Mtambuzi na Msajili wa Ardhi Shawana Sudi Khamis amewataka Wananchi watoe mashirikiano ya kutosha katika maeneo yao ili kulifanya zoezi hilo liweze kufanikiwa kama lilivyopangwa.
 
Ametaja baadhi ya faida zinazopatikana kwa kupitia zoezi hilo kuwa ni pamoja na kumuwezesha Mmiliki wa Ardhi kuwa na Ardhi Salama iliyothibitishwa na mamlaka rasmi za Serikali.
 
Itakumbukwa kuwa zoezi la Usajili na Utambuzi lilizinduliwa Rasmi Machi 28, 2013 ns Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Dkt ALI Mohamed Shein ambapo alipokea hati ya kwanza ya usajili wa Ikulu ya Zanzibar katika sherehe iliyofanyika Viwanja vya Viktoria Garden.
 
Utambuzi na usajili wa Ardhi ni hatua moja wapo ya kutekeleza Mkakati wa kupunguza umasikini Zanzibar  awamu ya pili ambao umeweka lengo la kusajili asilimia 50% ya ardhi ya Zanzibar ifikapo mwaka 2015.
 

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 22/08/2013

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>