Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk.Shein:Wakuu wa Mikoa na Wilaya Ieleweni Katiba na Sheria Kusaidia Utekelezaji wa Majukumu Yenu.

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakati akipokutana nao Ikulu Zanzibar.
 Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokutana na Rais Shein, Ikulu Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee, akizungumza wakati wa mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakati wa mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, Ikulu Zanzibar.


STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                      25 Oktoba, 2014
TAARIFA KWA VYOMBOVYA HABARI
Wakuu wa Mikoa na Wilaya wametakiwa kuisoma mara kwa mara na kuielewa Katiba pamoja na sheria nyingine za nchi kwa kuwa, wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku, wanapaswa kuzingatia Katiba na sheria hizo.
Wito huo umetolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati alifungua Mkutano Elekezi wa siku moja wa wakuu  wa Mikoa na Wilaya  za Zanzibar.
Alizitaja baadhi ya sheria ambazo wakuu hao wanapaswa kuzielewa na kuzitekeleza kila siku ni pamoja na Sheria Namb. 1 ya Mwaka 1998 ya Tawala za Mikoa, Sheria Namba 3 ya Baraza la Manispaa ya Mwaka 1995 na Sheria Namba 2 ya mwaka 2011 ya Utumishi wa Umma.
 Mbali ya kufahamu Katiba na Sheria Dk. Shein aliwataka pia wakuu hao wa mikoa na wilaya kuheshimu kiapo cha uaminifu wanachokula kabla ya kukabidhiwa dhamana zao na kuwakumbusha kuwa kiapo hicho ni jukumu walilochukua katika maisha yao ya hapa dunia na kesho kwa Mwenyezi Mungu.
 Aliwataka wakuu wa mikoa kuelewa kuwa wao ndio watendaji wakuu katika mikoa yao na kuwakumbusha mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ambayo yanaeleza kuwa wakuu wa mikoa na wilaya ni watendaji wa Serikali tofauti na ilivyokuwa kabla ya mabadiliko hayo.
 Dk. Shein aliwaeleza watendaji hao wakuu wa mikoa na wilaya kuwa shughuli za Serikali ni vigumu kutekelezwa katika ngazi hizo bila ya kuwepo kwao hivyo wanapaswa kuelewa uzito wa majukumu yao katika kuleta maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi katika mikoa na wilaya zao.
 Hata hivyo, amebainisha kuwa kazi za mikoa na wilaya si za kuratibu shughuli za Serikali Kuu pekee bali mikoa na wilaya inapaswa kuwa na dira na kupanga mipango yake ya maendeleo kwa kuzingatia changamoto, vipaumbele, mazingira na mahitaji ya mkoa na wilaya husika.
 Katika kufanya hivyo amewataka wakuu hao wa mikoa na wilaya kuzingatia pia Mipango Mikuu ya Maendeleo ya nchi ikiwemo Dira 2020, MKUZA Awamu ya Pili, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala- CCM ya Mwaka 2010-2015 pamoja na  Malengo ya Milenia.
 Dk. Shein amehimiza pia utendaji na uwajibikaji wa pamoja katika ngazi za mikoa na wilaya ambapo amesisitiza kuwa hiyo ndio njia muafaka katika kuleta ufanisi na tija hivyo kufanikisha utekelezaji wa malengo mbalimbali ya maendeleo.
 Katika maelezo hayo mafupi ya ufunguzi alikumbusha na kusisitiza pia umuhimu wa Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kutekeleza majukumu yao kwa kufuata maadili na miiko ya uongozi na kuwa mfano katika jamii.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee amewakumbusha wakuu wa Mikoa na Wilaya kuzingatia uwazi na uadilifu katika kutumia mamlaka waliyopewa kwa kuwa wanaweza kuwajibishwa kwa kutumia mamlaka hizo kinyume na maadili yanayokubalika.
 Akitoa mada katika mkutano huo, Dk. Abdulhamid alieleza kuwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kama watendaji wengine waliopewa mamlaka ya kuongoza hawana budi kuongoza kwa kuonesha njia na kuwa mfano mzuri wa tabia njema na utendaji.
 Katika mada yake hiyo Uongozi, Uwajibikaji, na Umuhimu wa Maadili katika Serikali za Mikoa na Wilaya aliwataka wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kutambua kuwa watumishi walio chini yao ndio rasilimali ya msingi hivyo hawana budi kuiheshimu, kuitunza na kuiendeleza.
 Kwa hivyo alisema kuwa watumishi hao wanapaswa kupewa fursa za kutoa mawazo na kuchangia katika kuendesha shughuli za serikali katika maeneo yao ya kazi na zaidi viongozi wawasikilize shida zao na kupewa misaada wanapohitaji kama inavyostahiki.
 Dk. Abdulhamid aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kusimamia nidhamu na maadili ya kazi na kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za kazi katika maeneo yao zinafuatwa kikamilifu.
Aidha, amewakumbusha kuhimiza umoja na mshikamano katika sehemu zao za kazi huku wakiwatumikia wananchi wote bila ubaguzi.  
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>