TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
01 Nov 2014
Ndugu waandishi wa habari ,
Kwanza napenda kumshukuru M/Mungu kwa mapenzi yake ya kutukutanisha hapa leo tukiwa wazima wa afya , pili napenda kuchukua fursa hii kukushukuruni nyie waandishi wa habari kwa kupoteza muda wenu na kuja kushirikiana na sisi , kwa hili tunawashukuru sana.
Ndugu waandishi wa habari,
Tuliopombele yenu ni viongozi halali wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) ambao tumechaguliwa kihalali tarehe 14/12/2014 kufuatia uchaguzi mkuu wa TAHLISO uliofanyika chuo cha Afya Bugando Mwanza, ambapo uchaguzi huo ulimchagua ndugu Mussa Mdede (Mwenyekiti), ndugu Abdi Mahamoud Abdi (Makamo mwenyekiti), ndugu Halima Bakari Nyange (katibu mkuu), ndugu Rajab Ali Rajab (Naibu katibu mkuu), ndugu Mollel Hillary (Mhazini) na ndugu Khamis Hamza Khamis (Mhazini Msaidizi).
Ndugu waandishi wa habari
Kwa mujibu wa katiba ya shirikisho la vyuo vikuu Tanzania (TAHLISO) ibara ya 5 (2) NI MARUFUKU kwa kiongozi yeyote haswa wa ngazi ya juu katika TAHLISO kushiriki katika shuhuli zozote za kisiasa haswa kupanda juu ya majukwaa ya kisiasa kwani kufanya hivyo nikuiwakilisha taasisi katika siasa wakati TAHLISO ni taasisi ya kijamii, lakini Mh. Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) ndugu Mussa Mdede alishiriki katika vugu vugu la siasa za vyama vingi kwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kalenga kufuatia kifo cha aliekua Mbunge wa jimbo hilo Mh. Marehemu Mgimwa
Ndugu waandishi wa habari,
Kwa kua katiba ya TAHLISO hairuhusu viongozi kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa tarehe 3 April 2014 katika chuo cha kodi jijini Dar es salaam.TAHLISO tulikutana katika kikao cha senate na kikao kiliamua kumuondoa madarakani ndugu Mussa Mdede kutokana na kuenda kinyume na katiba hiyo pia kikao kiliamua nafasi yake ikaimiwe na makamo mwenyekiti Ndudu ABDI MAHAMOUD ABDI mpaka pale Shirikisho litakapofanya uchaguzi mwengine au ikionekana kuna haja ya kufanya uchaguzi mdogo kabla ya uchaguzi wa December mwaka huu. Kwa kushangaza mara tu baada ya miezi sita kupita na kubadilika kwa viongozi katika serikali za wanafunzi katika vyuo mbali mbali Ndugu Mussa Mdede aliitisha kikao na kuwadanganya viongozi wapya wachache waliofika katika kikao hicho na kuendelea kujitangaza kwamba yeye ni mwenyekiti wa TAHLISO katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo tv na magazeti pamoja kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu kuandamana na kufanya migomo kwa ajili ya kuikomoa serikali.
Ndugu waandishi wa habari,
Hapa ndo tunataka mtutegee masikio yenu, vipaza sauti vyenu pamoja na kamera zenu kua Shirikisho la vyuo vikuu Tanzania TAHLISO na Shirikisho la vyuo vikuu Zanzibar ZAHILFE tunakemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa siasa nchini kuanzisha tabia mbaya ya kuwaita wanafunzi wa vyuo vikuu kisiri siri katika majumba yao, mahoteli mbalimbali na kupanga nao vikao vya siri, kualika viongozi wengi wa serikali za wanafunzi kutoka Tanzania bara kuja kushiriki mikutano mikubwa katika hoteli zilizopo Zanzibar ili kuweza kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kuwaunga mkono katika maadhimio yao. Shirikisho la vyuo vikuu nchini tunawaomba wanasiasa kuwacha tabia hiyo mara moja kwani tabia hiyo ndio iliyopelekea machafuko katika nchi mbali mbali duniani kama vile Libya, Bakhrein, Misri,Uturuki na nchi nyengine nyingi kuwataka wanafunzi kuandamana na kuwaahidi mambo mengi makubwa ambayo kiuhalisia hayatekelezeki na kuingiza nchi katika vita visivyo koma kama tunavyoona katika nchi kama vile LIBYA na MISRI katika kipindi hiki
Vile vile tunaziomba serikali zote mbili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo husika pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kulifuatilia suala hili na kulikataza mara moja kutokana na sababu kwamba amani ya nchi ikiondoka ni vigumu sana kuirudisha vile vile mambo haya yanaweza kuligharimu taifa kwa kupoteza wananchi wengi wasiokua na hatia.
Ndugu waandishi wa habari
MWISHO tunanapenda kuchukua fursa hii kuwaomba wanafunzi wote wa Tanzania kuitafuta katiba pendekezwa kuipitia na kuisoma katiba pendekezwa ya bunge maalum sura kwa sura ibara kwa ibara na neno kwa neno, ili kuifahamu na kuielewa na kuwacha kuwasikiliza wanasiasa ambao wanamalengo yao binafsi na ikifika april mwakani kuja kuipigia kura katiba hii kwa kua tulishirikishwa tokea mwanzo kwenye kutoa maoni ya mtu mmoja mmoja, vikundi, mabaraza na mwisho kushirikishwa katika hatua muhimu ya bunge maalum la katiba ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia taasisi zetu hizi ya ZAHILFE na TAHLISO tulitoa wawakilishi na kufaanikiwa kuingiza maoni yetu katika katiba na kueka historia ya taifa na kushiriki kuandaa misingi mizuri ya nchi yetu hususan katika vipengele vyote vinavyo ashiria kuufanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kua imara zaidi kwa kuziondoa kero zote za muungano huu uliodumu kwa muda wa miaka 50 sasa.
Imetolewa na:
Abdi Mahamoud Abdi
Makamo mwenyekiti TAHLISO