WASHIRIKI wa semina ya siku moja juu ya mazingatio ya uwezo wa kisiwa cha Pemba kupokea watalii, semina ilioandaliwa na hoteli ya Manta resort ya Makangaale na Kamisheni ya Utalii, ambapo ilifanyika ukumbi wa Weni Wete na kufunguliwa na waziri wa habari Zanzibar Mhe: Said Ali Mbarouk (picha Haji Nassor, Pemba)
MENEJA wa hoteli ya Manta resort ya Makangaale Micheweni Pemba Mathew Saus, akiwasilisha mada juu uwezo wa kisiwa cha Pemba kupokea watalii, kwenye semina ilioandaliwa na hoteli hiyo kwa pamoja na Kamisheni ya Utalii ambayo ilifanyika ukumbi wa mikutano Weni Wete Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
MKURUGENZI mkaazi wa ZIPA Pemba, Fadhila Hassan Abdalla akichangia mada juu ya maeneo yaliotengwa kisiwani Pemba kwa ajili ya utalii, kwenye semina iliofanyika ukumbi wa mikutano Weni Wete Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
WAZIRI wa Habari utamaduni, utalii na Michezo Zanzibar Mhe: Said Ali Mbarouk akifunga semina ya mazingatio ya uwezo wa kisiwa cha Pemba kupokea watalii, semina iliofanyika ukumbi wa Weni Wete, ambayo iliandaliwa na hoteli ya Manta resort na Kamisheni ya Utalii, kulia ni Kamishina wa Kamisheni ya Utalii Rabia Rashid Abdalla na kushoto na Mwenyekiti wa kamisheni hiyo dk Ahmada Hamad Khatib (picha na Haji Nassor, Pemba)