Saruji ikiwa ndani ya Gari , ambayo ililetwa Masjid Nuur na Uongozi wa PBZ Pemba, kwa kusaidia ujenzi wa mskiti huo.
Meneja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Haji Machano na Afisa wa Benki hiyo Pemba, Said Saleh kwa pamoja wakimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Masjid Nuur, Mtambile Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa mskiti huo
Jengo la msikiti ambao umesaidiwa na Wafadhili mbali mbali ikiwemo na PBZ Tawi la Pemba.
Picha na Bakar Mussa
Picha na Bakar Mussa
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),imeukabidhi Uongozi wa Msikiti wa Masjid Nuur , uliopo Mtambile Kisiwani Pemba, msaada wa Mifuko 100 ya Saruji yenye thamani ya Tshs, 1.4, Milion kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti huo.
Meneja wa Benk hiyo Tawi la Pemba, Haji Machano, aliwataka Wananchi Kisiwani humo, kuiunga mkono PBZ, kwa kuekeza fedha zao katika Benk hiyo kwani faida inayopatikana inawarejea Wananchi wenyewe kwa ajili ya maendeleo yao.
Alisema kuwa bado kuna baadhi ya wananchi wamekuwa hawana utamaduni wa kueka pesa zao Benk na hivyo kupelekea kuharibika kwa kuliwa na wadudu ama kuoza kwa maji na baadae kujuta kwa pale yanapo tokea matokeo kama hayo.
“ Nawaombeni Wananchi kutuunga mkono kwa kueka fedha zenu katika Benk yetu , kwani imekuwa na umahiri ,uzoefu ulio mkubwa wa kuhifadhi mali za wateja wetu, hivyo munapoweka fedha zenu aminini zitakuwa salama,” alisema Meneja.
Meneja huyo, alifahamisha kuwa kutokana na kuzingatia mahitaji ya Wateja wa Benk hiyo kuona kuwa faida inayopatikana kwenye Benk ni Riba, wamefunguwa Benk ya Kiislamu ambayo Matawi yake yako kila mahala ili kuwawezesha kuitumia fursa ya kuhifadhi Fedha zao katika maeneo salama.
Nae , Afisa wa Benk hiyo, Said Saleh Rashid, alisema PBZ, imekuwa ikitowa misaada mbali mbali kwa jamii kwa vile wanaimani kuwa Benk hiyo ni ya Wananchi wenyewe hivyo ni vyema kuitumia kwa faida yao.
Alieleza kuwa iwapo Wananchi wataitumia ipasavyo kwa kuweka amana zao itapiga hatuwa kubwa na hatimae kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii ya wananchi wa Zanzibar.
Mapema akipokea msaada huo Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Masjid Nuur , iliopo Mtambile Wilaya ya Mkoani , Salim Moh’d Hemed, aliipongeza Benk ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Pemba, kwa msaada wao walioutowa kwa ajili ya Ujenzi wa Msikiti huo na kuonesha kuwa Benk hiyo inajali maendeleo ya Wananchi .
Aliuahidi Uongozi wa PBZ, kwamba watautumia Msaada huo waliowapatia kwa haraka sana na kwa lengo lilokusudiwa kwani umewakombowa kwa kiasi kikubwa sana.
“Hatuna cha kuwalipa nyinyi Viongozi wa PBZ, kwani tulipo leta maombi yetu kwenu hamukutudhau mulitupokea na kutusaidia kile tulichoomba , kwa maana hiyo kwa kuthami juhudi zenu hizi ambazo Allah amewajalia tutautumia msaada huu kama ulivyokusudiwa” alisema kwa furaha.
Hivyo Mwenyekiti huyo, aliziomba taasisi nyengine ama watu wenye uwezo kuiga mfano wa PBZ, kusaidia maendeleo ya wananchi hasa yale yalionaishara ya kuwa endelevu kwa faida ya vizazi vilivyopo na vinavyokuja.