Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Mkoma akifungua Mkutano na Mablogger wa Tanzania kuzungumzia kukava habari za Uchaguzi na matukio mengine bila ya upendeleo, mkutano huo umewashirikisha Wamiliki wa Blog Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa mlimani city Dar-es-Salaam
Maofisa wa TCRA wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Pro. John Mkoma, akifunua mkutano huo katika ukumbi wa mlimani city. Mkutano huo umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania TCRA, uliofanyika katika ukumbi wa mlimani city.
Wamiliki wa Blog Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Mkoma akifungua mkutano huo uliozungumzia kuripoti habari za uchaguzi bila ya kupendelea Chama chochote na kutowa nafasi sawa katika kuripoti.
Eng Kisaka, kutoka TCRA akitowa Mada katika Mkutano huo uliowashilikisha Mablogger wa Tanzania jinsi ya kutumia Blog zao kutowa usawa katika kuripoti habari za Uchaguzi ili kuepuka na lawama kwa Jamii wanaofatilia mitandao ya Kijamii hutembelewa na Wananchi wengi na hufikisha habari kwa haraka sana kupitia Blog na kufuata maadili ya Uandishi wa habari.
Mablogger wakitafuta picha bora kupamba Blog zao ili kuvutia kwa Wadau wao wanaotembelea blog.
Mzee wa Blog,Bashir Nkoromo akichangia mada katika mkutano huo uliowakutanisha Mabloggers wa Tanzania katika ukumbi wa Mlimani City, ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Mdau wa Blog akichangika katika mkutano huo na kutowa Ushauri wake kufanikisha mitandao ya Kijami katika kuhabarisha kwa Jamii.
Mmiliki wa Blog ya Matukiodaima.blog.Ndg. Francis Godwin, kutoka Iringa alipota fursa kuchangia mada iliowasilishwa katika mkutano huo na Eng. Kisaka,wa TCRA,ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Umoja wa Mablogger Tanzania Mzee wa Matukio Francis Godwin
Mablogger wakifuatilia mkutano huo katika ukumbi wa Mlimani City. Mmiliki wa Blog ya mdimuz.Blog, Ndg. Henry Mdimu akichangia katika mkutano huo. Ni mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa Umoja wa Mablogger Tanzania baada kuchaguliwa Wajumbe Saba wakati wa mkutano huo.
Mmiliki wa Blog ya 8020fashiosblog.com, Bi Shamim Mwasha akichagia Mada iliowakilishwa katika mkutano huo na Eng Kisaka kuhusiana na kuripoti habari za Uchanguzi katika Blog. Bi Shamim Mwasha ni mmoja wa Wajumbe waliochaguliwa katika Kamati ya Muda ya Umoja wa Mablogger Tanzania. uliofanyika katika ukumbi wa mlimani city Dar-es-Salaam na kupata wajumbe saba kuunda kamati hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Profesa John Mkoma, akijibu maswali na michango ilioyotolewa na wamiliki wa Blog Tanzania, katika ukumbi wa mlimani City.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Tanzania Ndg. Asaa Mwambeni akifunga Mkutano wa Mablogger Tanzania uliotayarishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuzungumzia ukavaji wa stori katika Blog bila ya kupendelea kuchapisha habari hizo kwa usawa bila ya upendeleo kwa upande mmoja, na kuwaasa wamiliki wa Blog kutumia mitandao yao kuelimisha jamii na kuhabarisha ili kudumisha hali ya usalama na amani nchini
Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Ndg Assa Mwambeni akifunga mkutano huo wa mablogger, uliotayarishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kutowa elimu ya kuripoti habari za uchaguzi bila ya upendeleo kwa Chama kimoja
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Profesa John Mkoma akihojiwa na mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la BBC alioko Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa Mablogger wa Tanzania.