Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Waziri Kheri Afunga Mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Zanzibar

$
0
0
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                     13 Novemba,2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WASHIRIKI wa warsha ya mahusiano na mipaka kati ya viongozi wa kisiasa na kiutendaji wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata na kusisitiza kuwa mabadiliko makubwa yatarajiwe kutokea katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kuendelea kudumisha Muungano uliopo wa Tanganyika na Zanzibar.

Maelezo hayo waliyatoa katika ufungaji wa Warsha hiyo ya siku tatu iliyowashirikisha Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Maofisa Tawala wa Mikoa na Wilaya wa Zanzibar na baadhi kutoka Tanzania Bara iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Katika maelezo yao washiriki hao walieleza kuwa warsha hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutoa mwanga kwenye utendaji wao wa kazi sambamba na kuwa chachu katika kufikia malengo waliyojiwekea.

Walieleza kuwa mbali ya mafunzo walioyoyapata pia, warsha hiyo imeweza kujenga uhusiano na mashirikiano mazuri kati ya viongozi wa Mikoa wa Zanzibar na wale wa Tanzania Bara hatua ambayo itaimarisha zaidi Muungano uliopo kati ya pande mbili hizo.

Viongozi hao pia walipongeza juhudi za Dk. Shein katika kuwaletea maendeleo wananchi anaowaongoza sambamba na ushauri na miongozo mbali mbali anayotoa kwa viongozi akiwa na azma ya kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pamoja na hayo, viongozi hao walipongeza hotuba ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyotolewa na Dk. Shein ambayo walieleza kuwa ilikuwa ni dira katika mafunzo yao ya siku tatu.

Katika hutoba yake ya ufungaji, Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haji Omar Kheir aliwataka washiki kuitumia warsha hiyo kuwa ni fursa ya  kuendeleza, kuimarisha na kudumisha mashirikiano baina yao.


“Tushirikiane katika kubadilisha uzoefu kwa kutembeleana na pia, kuanzisha na kutekeleza mipango na program za pamoja kwa ajili ya kuwaletea maendeleo watu wetu katika maeneo yetu… mkutano huu uwe ni kichocheo cha kudumisha Muungano wetu”alisema Mhe. Kheir.

Aidha, Mhe. Kheir alisema kuwa  mafunzo hayo yamekuwa na umuhimu mkubwa sana kwani yameonesha njia na mbinu za kukabiliana na changamoto zilizopo baina ya viongozi wa kisiasa na kiutendaji katika Mikoa na Wilaya.

Alieleza kuwa lengo kubwa la warsha hiyo ni kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kueleza matumaini yake juu ya warsha hiyo ni kuwa waliyojifunza yatapelekea kufikia lengo hilo hali itakayothibitisha wazi pale itakapoonekana migogoro baina ya wanasiasa na watendaji imepungua ama kumalizika kabisa, ambapo ndiyo matarajio makubwa ya warsha hiyo.

Pia, alisisitiza kuwa mafunzo hayo yameongeza uelewa wa viongozi katika kutambua mipaka ya kazi zao, jambo ambalo litaimarisha Utawala Bora na kutoa wito kwa washiriki hao kwamba taaluma waliyoipata katika mafunzo hayo waitumie vyema katika kujenga mahusiano mazuri wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Sambamba na hayo, Mhe Kheir alieleza haja ya kuendeshwa warsha kama hiyo kwa Waheshimiwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ili kupunguza changamoto zinazojitokeza katika taasisi zao.

Akitoa neno la shukurani katika warsha hiyo  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa alieleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kwa kiasi kikubwa na kuahidi kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuleta mabadiliko makubwa katika utendaji wao wa kazi.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Comrade Said Mwambungu alieleza kuwa mbali ya mafunzo waliyoyapata katika hiyo, pia ushirikiano kwa viongozi wa Mikoa wa Tanzania Bara na Zanzibar nao umeweza kuimarika na kuahidi kuendeleza kushirikiana ili kuimarisha Muungano uliopo.

Katibu Mkuu  Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI  Jumanne Sagini alieleza azma ya  Wizara hiyo katika kutoa mafunzo kwa viongozi wake wote wakiwemo viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha wananfanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa. 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles