Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Ujumbe aliofatana nao Jaji Mkuu wa Tanzania alipofika kumjulia hali Rais Kikwete marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16,2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo
alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi, daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein Katanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama Ya Rufani Tanzania Mhe Ibrahim Juma ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyesindikiza msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali
jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda
kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland,