Baadhi ya wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi inazoshughulikia mambo ya Ukimwi wakimsikiliza Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF).
Wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi inazoshughulikia mambo ya Ukimwi waliohudhuria kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa kongamano hilo. Hadi sasa watoto wenye maambukizi ya VVU 130000 wameweza kufikiwa kati ya hao 39317 wamepewa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando wakati wa kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto linalofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF(Picha na Anna Mkinda - Maelezo Dar.)