Mhe Spika Anne Makinda ( Mb) akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dr. Theo-Ben Gurirab
Pamoja jukumu kubwa la mkutano wa kamati ya maandalizi, Mhe. Spika alipata nafasi ya kufika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo alipokelewa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi, Ramadhani Mwinyi. Hapa Mhe. Spika akisaini kitabu cha wageni na pembeni yake ni Balozi Ramadhan Mwinyi na aliyeketi ni Bw. Eliufoo Ukhotya kutoka Ofisi ya Spika
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, wajumbe wa kamati hiyo akiwamo Mhe, Spika Anne Makinda ( Mb) walikutana kwa siku mbili hapa Umoja wa Mataifa
Pamoja jukumu kubwa la mkutano wa kamati ya maandalizi, Mhe. Spika alipata nafasi ya kufika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo alipokelewa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi, Ramadhani Mwinyi. Hapa Mhe. Spika akisaini kitabu cha wageni na pembeni yake ni Balozi Ramadhan Mwinyi na aliyeketi ni Bw. Eliufoo Ukhotya kutoka Ofisi ya Spika
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, wajumbe wa kamati hiyo akiwamo Mhe, Spika Anne Makinda ( Mb) walikutana kwa siku mbili hapa Umoja wa Mataifa
Hapa ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson akisalimiana na Mhe. Anne Makinda ( Mb) Spika wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Na Mwandishi Maalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema, kutokana na dunia kukabiliwa na matatizo mengi na ambayo yanatokea kwa wakati mmoja.Kuanzia mlipuko wa Ebola, vita na machafuko , ugadi, uhalifu wa kupangwa na mabadiliko ya tabia nchi. Hakuna nchi ambayo inaweza kujidai kwamba inaweza kusimama peke yake.
Ameyasema hayo siku ya jumanne wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, mkutano utakaofanyika mwezi Agosti, 2015 Jijini New York.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ( Mb) ni kati ya wajumbe wa Kamati hiyo ya Maandalizi ambayo imekutana kwa siku mbili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Ban Ki Moon, amewaambia Maspika hao kwamba, dunia hivi sasa inakabiliwa na matatizo mengi sana na kuwa baadhi yake yanasababishwa kwa viongozi kutosikiliza sauti za wananchi wao.
“ kuna matatizo mengi yanayotokea na mengine yanatokea kwa sababu viongozi hawasikilizi sauti za wananchi wao. Kuna pengo kubwa kati ya wananchi na viongozi wao”. amesema Katibu Mkuu.
Na kwa sababu hiyo amesema, maspika wa mabunge na wabunge wao wanayonafasi kubwa ya kuepusha baadhi ya matatizo kwa kufikisha sauti na wananchi waliowachagua kwa viongozi wao.
Amesema bila ya ushirikiano ndani ya taifa kama nchi moja moja na katika ngazi ya kimataifa hakuna nchi ambayo inaweza kuhimili changamoto zinazotokana na matatizo ya aina yoyote ile.
“ Hakuna nchi inayoweza kusimama peke yake, wote lazima tushirikiane na kuwa kitu kimoja, lazima sote tuonyesha utashi wa kisiasa, tusaidiane kwa raslimali tulizonazo, tufanya kazi kwa pamoja ili kuyashaghulikia matatizo tuliyonayo” amesema Ban Ki Moon.
Akatoa mfano wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kama moja ya tatizo kubwa ambalo siyo tu limeleta madhara makubwa bali pia athari zake zimeleta mtikisiko mkubwa katika sekta nzima ya afya.
Amesema kutokana kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo na athari zake kiuchumi, kijamii na kimaendeleo ni wazi kwamba, pasipo kuwa na nguvu ya pamoja, ushirikiano thabiti wa raslimali tulizo nazo hakuna nchi iwe kubwa kiasi gani au ndogo inayoweza kujihakikisha usalama dhidi ya ugonjwa huo.
Akizungumzia nafasi ya Maspika na Mabunge wanayoyaongoza katika kukabiliana na matatizo yanayoikabili dunia hivi sasa iwe katika ngazi ya nchi husika au katika ngazi ya kimataifa. Ban Ki Moon alikuwa na haya ya kusema.
“ Nyinyi mnawakilisha wananchi waliowachagua, mnawakilisha sauti zao, ninayoheshima kubwa sana kwenu pamoja na kazi mnazozifanya”
Akawachekesha maspika hao kwa kusema, katika maisha yake yote ya utumishi hajawahi kufikilia kuwa mbunge ingawa amekuwa na uhusiano mzuri na wanasiasa.
Amesema pamoja na kuwa wawakilishi wa wananchi, wabunge ndio wanaopitisha bajeti za serikali zao ikiwa ni pamoja na kupitisha mikataba ya kimataifa.
Na hivyo amewataka wabunge hao kushirikiana kwa karibu na serikali zao na hasa katika kupindi kijacho ambacho serikali zitakuwa zikijianda na utekelezaji wa ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015.
“ Hata kama serikali zitakuwa na mipango mizuri , kama bunge halitapitisha bajeti inayotakiwa ni wazi kwamba mipango hiyo haitaweza kutekelezwa kwa ukamilifu, kwa hiyo moja ya rai yangu kwenu shirikianeni na serikali ili muweze kuwaletea wananchi wenu maendeleo endelevu” amesisitiza Katibu Mkuu.
Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw Jan Eliasson akibadilishana mawazo na wajumbe wa kamati hiyo ya Maandalizi amesema hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu lakini kila mtu anaweza kufanya jambo fulani.
Naibu Katibu Mkuu katika mazugumzo yake pamoja na mambo mengine ametilia sana mkazo umuhimu wa amani, usalama, utawala wa sheria na demokrasia kama baadhi ya nguzo za maendeleo.
Akasema yapo mambo muhimu ambayo mwananchi wa kawaida anayataka ambayo ni amani, maendeleo, serikali na taasisi anazoziamini, ushiriki na sauti yake kusikika katika mambo yenye maslahi kwake.
“ Wananchi wanatuangalia sisi viongozi wao, je tunawashuri ipasavyo, je tunazingatia maslahi yao. Wananchi wa leo siyo wale wazamani, wanauelewa na ufahamu mkubwa wa mambo yanayowazunguka na teknolojia ya mawasiliano imewaongezea uelewa huo. Wanajua nini wanachokitaka na nini wanakitarajia kutoka kwa viongozi wao” amesisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Amewataka Maspika, wabunge pamoja na mihimili mingine ya dola kuwa na mtizamo mpya na fikra mpya na pana zaidi za siyo tu kushughulikia matatizo ya wananchi wao lakini pamoja na matatizo mbalimbali yanayoikabili dunia hivi sasa.
Na kuongeza kuwa kila mtu katika nafasi yake iwe serikali, bungeni, katika sekta binafsi au katika asasi zisizo za kiserikali anaowajibu anaotakiwa kuutekeleza. Na kwamba makundi hayo na mengine mengi ya kijamii kwa umoja wao yanatakiwa kuingia katika kipindi kipya cha ushirikiano na mshikamano.