Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Uchunguzi Hospitali ya Mnazi Mmmoja Dk Msafiri Marijani, akitowa shukrani kwa Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipa Kodi TRA Ndg. Richard Kayombo na Ujumbe wake walipofika kutowa Msaada wa Vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 20.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Uchunguzi Dk. Msafiri Marijan akitowa shukrani kwa msaada huo uliotolewa na TRA kwa hospitali ya Mnazi mmoja wenye thamani ya shilingi milioni 20, Vifaa vilivyokabidhiwa magodoro mia moja na mashuka yake 100, Mapazia ya kukinga mgonjwa akihudumiwa akiwa wodini na vifaa vya Oxygen vitatu. kwa ajili ya kutowa huduma kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Wateja TRA, Ndg. Richard Kayombo, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya hospitali ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania yenye kauli mbiu yenye Ujumbe wa Risiti Haki Yako Mteja, wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Naibu Kamishna wa TRA Zanzibar Ndg Mcha Hassan, akizungumza na kufafanua jambo wakati akiulizwa swali na waandishi wa habari kujua makusanyo ya Kodi.
Maofisa wa Hospitali ya Mnazi Mmoja wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya msaada uliotolewa na TRA kwa ajili ya Hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Wateja TRA, Ndg. Richard Kayombo,(kulia) akimkabidhi vifaa Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk. Jamala Adam.Talib, moja ya vifaa hivyo vilivyotolewa na TRA, kwa ajili ya hospitali hiyo. Vifaa vilivyokabidhiwa ni Magodoro na Mashuka mia Mapazia ya kutowa huduma mgonjwa na Vifaa vya Oxgeny 3, makabidhiano hayo yamefanyika hospitali ya mnazi mmoja.kushoto Naibu Kamishna wa TRA Zanzibar Ndg, Mcha Hassan na katikati Dk. Marijani