Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif : Uchaguzi 2015 utakuwa wa utulivu na wa amani

$
0
0
Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo la Kituo cha Afya cha Jimbo la Mtoni ambalo lililoanzishwa kwa mchango wa Wananchi na Viongozi waliopita wa jimbo hilo.

ijana wa matambuizo wa Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Mtoni wakifanya vitu vyao wakati wa mkutano wao na Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Balozi Seif aliyefanya ziara kukagua maendeleo ya Chama Mkoani humo.




---
Wanachama wapya 50 wa Chama cha Mapinduzi na Jumuia zake wa Jimbo Jimbo la Fuoni wakila kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa kadi kwenye mkutano wa hadhara hapo Tawi la CCM Pangawe.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.



Na Othman Khamis Ame, OMPR

Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Kichama ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amewahakikishia wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwamba uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 unatarajiwa kuwa wa utulivu na amani.


Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya dola vitahakikisha kuwa vikundi vya kihuni vinavyoanza kuandaliwa kwa ajili ya kuvuruga uchaguzi huo itapambana navyo kwa nguvu zake zote.

Balozi Seif Ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza hayo wakati akihutubia Mkutano wa hadhara baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ndani ya  Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa mlezi wa CCM Mkoa huo, Mkutano  uliofanyika katika uwanja wa Kwamabata Magogoni.

Alisema wananchi walio wengi wameshuhudia vitendo vya kihuni vilivyofanywa na vikundi vya Vijana kujaribu kuvuruga zoezi la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu mambo ambayo alisema hayatokubalika kutokea tena kwenye uchaguzi Mkuu ujao hapo mwakani.


“ Wananchi wameshuhudia uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu jinsi ulivyokumbwa na vikundi vya kihuni  vilivyoandaliwa kwa makusudi kujaribu kuharibu kwa makusudi zoezi la uchaguzi huo“. Alisema Balozi Seif.

Aliwaomba wafuasi wa vyama vya upinzani hapa Nchini kuamua mapema kufuata chama chenye muelekeo wa kuleta maendeleo ya wananchi ambacho kwa hivi sasa ni chama cha Mapinduzi.

Alifahamisha kwamba ushindi wa chama cha mapinduzi mwaka 2015 hauna mbadala kutokana na ilivyojipanga na kuungwa mkono na wananchi walio wengi hapa Nchini.

“ Gari ya ushindi inaanza kuondoka waiwahi mapema wasije fikia wakati wakaanza kujilaumu wenyewe  wakati mtete wao atakuwa hayupo“. Alieleza Balozi Seif.

Aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi  wote kujiepusha na wimbi la vikundi vilivyojikubalisha kujiingiza katika vitendo vya ugaidi ambayo kamwe havikubaliki Kitaifa wala Kimataifa.

Alisema Serikali zote mbili kupitia vyombo vote vya dola zitakuwa makini kufuatilia mienendo ya watu hao na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Katika Mkutano huo wa hadhara Balozi Seif ambae pia ni Naibu Kamanda wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania aliwatawadha makamanda wa Vijana wa Majimbo na Wilaya zilizomo Mkoa wa Magharibi Kichama baada ya kuteuliwa na Baraza Kuu la UVCCM.

Makamanda aliowatawadha ni Mh. Thuwaiba Kisasi Kamanda wa Mkoa wa Magharibi,Kanal mstaafu Masoud Khamis Wilaya, Ibrahim Ramadhan Jimbo la Mtoni, Fatma Adam Jimbo la Bububu, Bimkubwa Nassor Jimbo la Mfenesini, Ibrahim Raza Jimbo la Dimani, Hafidh Tahir Ali Jimbo la Fuoni, Ahmada Abdullwakil Jimbo la Mwanakwerekwe na Abass Hassan Juma Jimbo la Magogoni.

Balozi Seif aliwapongeza Makamanda hao wakiashiria dalili njema ya kuwalea vyema Vijana ili wawe na mwamko mkubwa wa kukipenda na kuendelea kukiunga mkono chama cha Mapinduzi.

Mapema asubuhi akizungumza katika Kikao cha Majumuisho ya ziara yake ya siku mbili akiwa mlezi wa CCM wa mkoa wa Magharibi  hapo Tawi la CCM Mbweni Balozi Seif aliwataka Viongozi wa kamati za siasa za Matawi hadi Mkoa kutoogopa au kusemwa wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Alisema ni vyema kwa  viongozi hao kuwatumia zaidi Vijana  katika kuongeza nguvu za   kuimarisha utekelezaji wa ilani na sera za chama ikitoa pia fursa kwao kupata wasaa wa kujitathmini katika ngazi wanazoziongoza.

Balozi Seif aliwatahadharisha Viongozi hao kujiepusha na tabia ya kujiingiza katika masuala ya rushwa ambayo yameelezwa wazi  na kuonywa katika ahadi za Chama cha Mapinduzi kwa vile hatma yake huvuruga maadili yote ya  uwajibikaji.

Alitolea mfano nafasi za uwakilishi na Ubunge akisema kwamba ni kazi zilizoundwa katika mfumo wa Kidemokrasia za kuhudumia jamii lakini kinyume na hivyo ni kuwatesa na kuwanyanyasa Wananchi.

Alifahamisha kwamba vitendo vya kutumia ubabe, fitna na  majungu  katika kuomba nafasi za Uongozi  zinachangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga amani na kuwagawa wananchi.

Akimkaribisha Mlezi wa CCM Mkoa huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf aliwaasa wananchi wa Majimbo ya Magogoni na Mtoni kujiepusha mapema na madhila pamoja na matatizo waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Mwenyekiti Yussuf alisema njia pekee ya kuondokana na madhila hayo ni kwa wananchi hao kukipigia kura chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>