Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk Shein : Tutafuatilia malalamiko dhidi ya ajira za Polisi

$
0
0
---
STATE HOUSE ZANZIBAR

---OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE
---
    Zanzibar                                                             02 Disemba, 2014


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi kufuatilia tuhuma za kuwepo kwa vitendo vya baadhi ya wananchi kudaiwa fedha wakati wa zoezi la kuteua vijana kujiunga na jeshi la Polisi kisiwani Pemba hivi karibuni.

“nitafuatilia tuhuma hizo ili waliofanya hivyo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Si mara ya kwanza kusikia matukio kama hayo na yanapotokea tumekuwa tukiyafuatilia na kuchukulia hatua” aliahidi Dk. Shein.

Dk. Shein alisema hayo leo huko Micheweni wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa mashina na maskani za Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya hiyo ambapo madai hayo yalielezwa na mmoja wa viongozi hao kuwa baadhi ya vijana alitakiwa kutoa fedha ili awapate nafai za kujiunga na jeshi hilo.

Rais wa Zanzibar ambaye alionekana kushtushwa na taarifa hizo wakati huu ambapo Serikali anayoiongoza imedhamiria kupambana na rushwa na uhujumu wa uchumi, alisema alitamani angekuwa anamfahamu aliyetenda kitendo hicho ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hata hivyo Dk. Shein aliwaasa wazazi kuwaandaa na kuwashajiisha watoto wao kutumia fursa zilizopo za kujiajiri badala ya kutegemea kazi za kuajiriwa ambazo hazipo za kutosha.

“wazazi lazima tuwaandae vijana wetu kujiajiri badala ya kusubiri ajira. Serikali inazidi kujidhatiti na kujiimarisha kuwawezesha vijana kujiajiri katika kazi wanazozichagua kwa kutoa fursa za mikopo kupitia mifuko iliyopo” Dk. Shein alisema.

Katika mkutano huo, Dk. Shein aliwataka wazazi kuwahimiza watoto wao waliofikia umri wa kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kufanya hivyo bila kukosa ili wakati ukifika waweze kutumia haki ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wao.

Alisisitiza pia umuhimu wa wazazi kuwaelimisha watoto wao historia ya Zanzibar na kuwataka kuzingatia historia hiyo ambayo inaonesha Zanzibar ilitawaliwa karibu miaka mia nne hadi kufanyika kwa Mapinduzi ya mwaka 1964.



Alibainisha kuwa tangu Mapinduzi hayo Zanzibar imeweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo ingawa alikiri kuwa kutokana na ongezeko kubwa la watu kumekuwepo na changamoto nyingi za kimaendeleo ambazo serikali imekuwa ikichukua hatua za kukabiliana nazo.    

Akizungumza katika Mkutano huo Naibu Katibu  Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai aliwataka wana CCM Pemba kuhakikisha kuwa wanakabiliana na upotoshaji wa makusudi wa Katiba Iliyopendekezwa unaofanya na wapinzani.

---Alisema Katiba hiyo imezingatia maslahi ya pande zote za Muungano na kubainisha kuwa wanaopinga ni nia yao sio tu kuwa ni kuzorotesha muungano bali kuuvunja kwa maslahi yao binafsi.  

Katika risala yao viongozi hao walipongeza uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya uliofanywa  hivi karibuni na Mhe Rais na kueleza kuwa mabadiliko hayo yameleta matumaini mapya katika mkoa na wilaya yao.

Risala hiyo ambayo ilisomwa na Mariam Omar Ali ilieleza mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo ambapo ilieleza kuwa karibu kila shehia imeweza kupata huduma za jamii ikiwemo maji safi na salama, umeme, elimu, afya, na mawasiliano.

Wakati viongozi hao walipopata fursa za kutoa maoni yao katika mkutano huo baadhi walieleza wasiwasi wao juu ya kasi inayoongezeka kila siku ya baadhi ya watu kutoka nje kuja kisiwani Pemba na kuwasilisha nyaraka za kudai mashamba na kukubaliwa na baadhi ya maofisa wa serikali.

Dk. Shein ambaye anatarajiwa kuendelea na ziara yake kesho kwa kutembelea wilaya ya  Chakechake amefuata na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai, Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwemo mawaziri.


Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>