Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yahya Khamis Hamad, akifungua mkutano wa Mjadala wa Mchakato wa Katiba,(Bunge la Katiba) ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar katika ukumbi wa Ecrotanal Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Profesa Chris Maina Peter, akitowa maelezo kuhusiana na Mjadala huo uliowashirikisha Wadau mbalimbali Zanzibar.kuchangia uundwaji wa (Bunge la Katiba).
Washiriki wa Mjadala wa Mchakato wa Katiba (Bunge la Katiba) wakimsikiliza Mtoa mada ya akiwasilisha mada kisheria kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya Tanzania.
Mwanasheria Ali H.Ali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mkuu Zanzibar, akitowa Mada katika mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria Zanzibar, kuhusu mjadala wa mchakato wa Katiba (Bunge la Katiba ).katika ukumbi wa Ecrotanali Zanzibar.
Mwanasheria Suleiman Masoud kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, akiwasilisha mada kuhusiana na Mjadala wa Mchakato wa Katiba (Bunge la Katiba ).
Washiri wa Mjadala wa Katiba wakimsikiliza mtoa Mada katika mkutano huo wa Mjadala wa Mchakato wa Katiba Tanzania ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
Mwakilishi wa jumuiya ya Watu wasiosikia hutumia Alama za Ishara akichangia katika mjadala huo kuhusu kusahauliwa Watu wa mahitaji maalum kutokushirikishwa.
Kiongozi wa Chama cha Siasa Mchenga akichangia na kufafanua kifungu cha 22 cha uundaji wa Bunge la Katiba kufanyiwa marekebisho
Wachangiaji wengi katika Mjadala wa Mchakato wa Katiba kuhusu Bunge la Katiba wamechangia katika kifungu cha 22 cha uungwaji wa Bunge la Katiba na kutaka kufanyiwa marekeshisho na kuondoa baadhi ya vifungu na uwiano wa Wajumbe wa Bunge la Katiba katika uundwaji wake.na kuwashirikisha Vijana na Watu wenye mahitaji maalum.
Mwananchi akichangia Mjadala wa Mchakato wa Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar. na kuwashirikisha Wananchi wa taasisi mbalimbali za jamii. na serekalini na vyama.
Mshiriki wa Mjadala wa Mchakato wa Katiba Rashid Joe akichangia katika mjadala huo kuhusu vifungu vyakuunda bunge la katiba,mchakato huo umefanyika katika ukumbi wa jengo la Ecrotanal maisara.
Mshiriki waMjadala huo akichangia kifungu cha sheria cha uungaji wa Bunge la Katiba.
Wananchi wamepata ushiriki kwa mpeo mkubwa wa kuchangia Mjadala wa mchakato wa Katiba mpya Tanzania, mjadala huo umetayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
Fursa ya kuchangia Mjadala wa Katiba ya uundaji wa Bunge la Katiba,Mshiriki Dadi Kombo akichangia kifungu cha 22, juu ya uundwaji wa Bunge la Katiba, wakati wa mjadala wa Katiba uliotayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
Nao akina Mama nao wamepata fursa ya kuchangia katika mjadala wa mchakato wa Katiba, katika mkutano wa mjadala wa Katiba kuhusu uungwaji wa Bunge la Katiba.
Mwananchi akichangia Mjadala wa Katiba kuhusu Bunge la Katiba.
Mwananchi Rashid akichangia Mjadala wa Katiba Mpya, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.na kuwashirikisha wadau na Wanaharakati mbalimbali Zanzibar.