Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ajifungua barazani baada ya kunyimwa kitanda hospitali

$
0
0
Na Kija Elias, Moshi
Wauguzi wa zamu katika kituo cha afya cha Pasua kilichopo manispaa ya Moshi, wanatuhumiwa  kumtolea lugha chafu mama mjamzito ikiwemo pia kumnyima kitanda na hivyo kujifungulia nje ya baraza ya nyumba ya jirani  muda mfupi baada ya kufukuzwa kituoni hapo.

Mama huyo Josephine Michael (21), mkazi wa kata ya Kaloleni, manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikumbwa na mkasa huo Novemba 29 mwaka huu, baada ya kufika kituoni hapo kwa ajli ya kupatiwa msaada wa kujifungua lakini katika hali isiyokuwa ya kiutu aliambulia kufukuzwa na wauguzi hao wa zamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mama huyo alisema baada ya kufika katika kituo hicho cha afya,  majira ya saa mbili usiku na kuwaeleza wauguzi hao wa zamu  juu ya kile kilichokuwa kinamsibu, alielezwa kuwa hakuna kitanda kwa watu ambao si wagonjwa.

Alisema baada ya kuambulia majibu hayo, aliondoka kurejea nyumbani kwake na alipofika nyumbani hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na hivyo kukimbilia kwa majirani kuomba msaada ambapo kabla ya kupatiwa msaada huo na majirani mfuko wa uzazi ulipasuka.

Miongoni mwa waliojitoa muhanga kuokoa uhai wa mama huyo pamoja na mtoto wake ni mwandishi wa habari, Safina Sarwatt (Mtanzania), ambaye alilazimika kutumia mwanga wa simu yake ya kiganjani kumzalisha mama huyo akishirikiana na majirani zake.


“Mama huyo alikuja kwenye kibaraza chetu huku akiomba  msaada wa kujifungua, tulipo mwangalia tulimkuta yupo katika hatua za mwisho kujifungua  ndipo tulipotoka na kumtandikia khanga chini na kuanza  kumsaidia ambapo alifanikiwa kujingua mtoto wa kiume akiwa salama,”alisema Sarwatt.

Sarwatt alisema licha ya kutokuwa na utaalamu wowote aliendelea kutoa msaada huo na kumkimbiza katika kituo cha afya cha Pasua.

 “Tulipomaliza kumzalisha mama huyo tulilazimika kufunga kitovu  cha mtoto kwa kutumia mfuko wa rambo, kutokana na kutokuwa na vifaa tiba na kisha kumkimbiza hospitali kwa matibabu zaidi,”alisema.

Aidha alisema wakati wakimpatia msaada huyo, umeme ulikatika na hivyo kuwa na giza ndipo walipolazimika kutumia mwanga wa simu ya kiganjani ili kumsaidia mama huyo asipoteze uhai wake.

Akizungumza mama huyo akiwa katika kituo cha afya cha Pasua wodi ya watoto, alimpongeza mwandishi huyo kwa kuwa na moyo wa kipekee  kwani ni watu wachache ambao wanaweza kujitolea.


Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Moshi,Shaaban Ntarambe, hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo kwa kile alichodia suala hilo ni la kitaalamu na kuwataka waandishi wa habari kuandika maswali ili ayawasilishe kwa wataalamu wake wa idara ya afya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>