Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ulemavu si mzigo, asema Mazrui

$
0
0
Na Haji Nassor, Pemba
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazuri, ameitaka jamii kuacha dhana potofu ya kuwaona watu wenye ulemavu kama mzigo, wakikumbuka kuwa huo ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Alisema jamii sasa imekuwa ikichupa mipaka na kujilaumu na wengine kuona haya hata kuwatoa nje mtoto mwenye ulemavu na kusahau kwamba hakuna alieomba kuzaliwa akiwa hivyo.

Alitoa kauli hiyo jana uwanja wa Tenis mjini Chake Chake Pemba, kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani, ambapo kitaifa kwa Zanzibar yalifanyika kisiwani humo.

Alisema sio sahihi kwamba watu wenye ulemavu hawana mchango wowote kwenye jamii, ambapo dhana hiyo husambazwa na makundi ya wachache ambao hawana ubinaadamu.

Alisema ipo mifano hai ndani ya serikali na hata taasisi binfasi, kwamba watu wenye ulemavu wamefanikisha mambo makubwa na kufuta majina wanayopewa kwamba ni mzigo kwenye jamii.

“Mimi siamini kwamba watu wenye ulamvu ni mzigo kwenye jamii, maana hata kwenye kampuni yangu, yuko mlemavu ambae anafanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa, sasa wanaosema ni mizigo hao wamepitwa na wakati,” alisema.

Katika hatua nyengine waziri huyo alisema serikali imekuwa ikijitahidi kuweka mazingira mazuri ili kuona watu wenye ulemavu wanapata haki na fursa sawa.

Alisema hata uwepo wa sheria namba 9 ya mwaka 2006 ni miongoni mwa hatua thabiti ambayo kwa sasa imeweka mazingira imara sambamba na kuwapatia vifaa.


Akisoma risala ya watu wenye ulemavu wa mikoa mitano ya Zanzibar, Msataafu wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu (UWZ) Atie Suleiman, alisema watu wenye ulemavu wamekuwa mara nne ya wananchi wanaokumbwa na majanga kuliko wengine wasiokuwa na ulemavu.

“Lazima serikali ituandalie kutupa mazingira mazuri, maana yanapotokezea majanga na mafuriko sisi huathirika mara nne kuliko wengine,” alisema.

Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano yalioanza ofisi za Zantel mjini Chake Cake na kupokelewa na waziri huyo.

Kuna watu bilioni moja wanaoishi na ulemavu duniani na kwanza watu wenye ulemavu wamefikia 16,533.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>