Katibu wa Kamati ya Bandari ya Nyanjale Kiomba Mvua Bwana Moh’d Ali akitia saini makubaliano yaliyofikiwa baina ya Wanakijiji hicho na Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff iliyopo Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Waliosimamanyuma yake wakishuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kana Mstaafu Juma Kassim Tindwa, Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Mh. Makame Mshimba Mbarouk, Mwanasheria wa Makamu wa Pili Bibi Mwanaisha Shamte,Menaja Mkuu wa Sea Cliff Bwana Abre Esterhuizen na Mwanasheria wa Wizara ya Ardhi Nd, Khamis Faraji.
Wajumbe wawili wa Kamati ya Bandari ya Kiomba Mvua Bwana Othman Ashkina na Bibi Chiku Sheikh wakimwaga wino kwenye maridhiano waliyofikia na Hoteli ya Sea Cliff.Wajumbe hao wanashuhudiwa nyuma na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji na Afisa Tawala Wil;aya ya Kaskazini B Nd. Juma Abdulla.
Sheha wa Shehia ya Kiomba Mvua Bwana Mzee Ramadhan Mzee akitia saini kama shahidi Makubaliano ya maridhiano kati ya Wananchi wa Kiomba Mvua na Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Abre Esterhuizen akimwaga wino kwenye maridhiano hayo ya makubaliano na wana Kijiji cha Kiomba Mvua.
Menaja Utawala na Uendeshaji wa Hoteli ya Sea Cliff Bwana Abdulmalik Mussa Kushoto na Meneja wa Mchezo wa Golf wa Hoteli hiyo Bwana Heirz Papenfus wakijumuika kutia saini Mkataba huop wa maridhiano.
Balozi Seif akimpongeza Katibu wa Kamati ya Bandari ya Nyanjale Kiomba Mvua Bwana Moh’d Ali mara baada ya kumalizika kwa zoezi la utiaji saini mkataba wa maridhiano kati ya Uongozi wa Hoteli ya Sea Cliff na Wana Kijiji wa Kiomba Mvua.(Picha na Hassan Issa OMPR)