Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wawakilishi, Masheha hawana Nafasi Awamu ya Tatu ya TASAF.

$
0
0
Na Haji Nassor, Pemba
WABUNGE, Wawakilishi, Madiwani,Masheha na viongozi ngazi ya mkoa, hawatakuwa na nafasi tena ya kuwachukua watu wawatakao, ili wawezeshwe katika awamu ya tatu ya mradi wa TASAF.

Hayo yalielezwa jana na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha TASAF, Zuhura Mdungi, wakati akiwasilisha mada juu utaratibu na mpango wa utekelezaji, kwenye warsha ya siku mbili ya utekelezaji wa miradi yaTASAF awamu ya tatu.

Alisema kwa vile awamu ya tatu ya TASAF imekusudia kwenda mbali zaidi kwa kuziwesha kaya masikini, hivyo viongozi hao kuanzia sasa wasitarajie kupata fursa ya kuwaingiza ndugu na jamaa kupata fedha.

Alisema hilo litazuilika kutokana na mfumo mpya uliobuniwa na TASAF wa kieletroniki ambao moja kwa moja hautaruhusu kuchezewa na viongozi hao kwa matakwa yao binafsi.

Alisema lengo la TASAF ni kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa kwa kuzifikia kaya maskini zaidi.

Akifungua warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Meja (mstaafu) Juma Kassim Tindwa, amewataka Madiwani na masheha kuhakikisha wenyewe wanaimarisha umoja na mshikamano wao, ili wananchi wapate hamasa ya kuitekeleza miradi yao ya maendeleo.

Alisema TASAF awamu ya pili, ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na wananchi kuamua kuzika tofauti zao, jambo ambalo hata viongozi nao waliamua kufanya hivyo.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa TASAF Taifa, Ladislaus Mwamanga alisema, wakati umefika kwa kaya masikini zaidi za Tanzania, kujiweka tayari kwani TASAF imekusudia kuwapunguzia umasikini kwa kiwango kikubwa.

Akizugumza nje ya ukumbi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, alisema kwa upande wa kisiwa cha Pemba, TASAF imelenga zaidi eneo la ukanda wa mashariki wa kisiwa hicho.

“Kwa kweli kisiwa cha Pemba, TASAF inaelekeza guvu zake hasa ukanda wa mashariki wa kisiwa ambacho inaonekana umasikini umekithiri,’’ alifafanua Dadi.

Katika awamu iliyomalizika TASAF ilitekeleza miradi 366 kisiwani Pemba ikiwemo ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha kifusi, ufugaji, uvuvi, ambapo jumla ya shilingi bilioni 6.22 zilitumika.

Wakati huo huo, Hafsa Golo anaripoti kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga alisema mrdai huo umepanga kuwafikia walengwa milioni 1.5 katika kaya hizo.

Alisema lengo ni kuzinusuru kaya hizo na umasikini hasa zile ambazo zimo katika mazingira hatarishi katika vijiji na mitaa.

Aidha alisema miongoni mwa utekelezaji wa miradi ni kuangalia sekta ya sfya,elimu na maji.

Hata hivyo alisema awamu ya pili ya mradi kuna mapungufu mengi yamejitokeza hivyo aliwataka wadau kurekebisha kasoro ili malengo yaweze kufikiwa.

Mapema akifungua warsha hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya uongozi TASAF kwa upande wa Unguja, Abdalla Mwinyi, aliwataka wajumbe wa mkutano kwenda kuelekeza na kuitekeleza kikamilifu mionngozo na taratibu ambazo wamepewa katika mradi huo kwa wanajamii.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>