Na Mwandishi wetu, Dodoma
KAMATI Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa itakutana leo ikifuatiwa na Halmashauri Kuu kesho katika kikao cha siku mbili.Katika kikao hicho, Kamati Kuu itajadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa white house Dodoma, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Pia kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na masuala utumishi.
Alisema Jumamosi asubuhi kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua baraza la ushauri la wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.
Baraza hilo linaundwa na wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu wa CCM taifa.
Mwandishi wetu Mwantanga Ame alieko Dodoma anaripoti kuwa tayari Wajumbe wengi wa mkutano huo wakiwemo kutoka Zanzibar wameshawasili Mjini Dodoma kuhudhuria kikao hicho.