Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemhamisha Mhandisi Ibrahim Iyombe, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya ujenzi.Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema Eng. Iyombe anachukua nafasi ya Mhandisi John Stanslaus Ndunguru ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha, taarifa imesema kuwa uhamisho huo unaanza mara moja.