Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Jiji la Sundsvall lililoanzisha mahusiano na wadi za Makunduchi

$
0
0
Hili ni jiji la Sundsvall nchini Sweden. Mji huu unaoendeshwa na manispaa ya Sundsvall umeanzisha mahusiano na wadi za Makunduchi yenye lengo la kuiweka Makunduchi kwenye ramani ya dunia kwa upande wa elimu. Mji huu umeanzishwa mwaka 1621 na mfalme Gustav ll Adolf ambaye alikuwa kiongozi shupavu kijeshi.
 
Lengo la mtawala huyu ni kuigeuza Sweden kuwa dola yenye nguvu duniani. Kiuchumi mji huu ulitegemea kuuza mbao. Hata nyumba zake za enzi hiyo zilikuwa za mbao. Mwaka 1888 mji huu uliteketezwa kwa moto na kubakia jivu tupu.
 
Hali hii ilipelekea kuachana na ujenzi wa nyumba za mbao katikati ya jiji na hapo ndipo jina la mji wa mawe (stone city) likajitokeza. Mabigwa wa ujenzi kutoka nchi mbali mbali za Ulaya waliingia Sundsvall kujenga nyumba za Mawe ambazo hadi leo zinaonekana mjini hapa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>