Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dk Shein : Serikali itahakikisha sekta ya biashara inaimarika ili kuleta maendeleo

$
0
0
Ali Issa na Mariam Himid-Maelezo
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha sekta ya biashara,viwanda,masoko na uwekezaji inaimarika kwa kiwango kikubwa ili kuleta maendeleo hapa Nchini.
 
Hayo ameyasemaleo huko Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Baraza la Biashara la Taifa la Zanzibar lililojumuisha sekta mbalimbali za kibiashara, viwanda na uwekezaji.
 
Amesema katika kulifikia hilo Serikali itashirikiana na sekta binafsi ili kuona kua sekta hiyo inaimarika na kupiga hatua kubwa kiuchumi.
 
 “lazima kuwepo mazingira mazuri ya biashara na kufuata utaratibu mzima ulio wekwa,wafanya biashara hawapendi kuona wanafanyiwa urasimu,kutoa rushwa na mengineo,mambo haya yapo na simazuri kufanyika.,alisema Dkt. Shein akiwa ni mwenyekiti wa Mkutano huo.
 
Aidha alisema kuwa Serikali hivisasa inahitaji kufikia mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji hapa Nchini, hivyo sekta husika zinazo fanikisha halihiyo ni jukumu lao kilammoja kuondosha kero zinazo wakumba wafanya biashara na waekezaji.


Nao wajumbe wa Baraza hilo walimuomba mwenyekiti wa baraza hilo kuondolewa urasimu uliopo pale ambapo muekezaji anapotaka kuekeza na kupatiwa hati ya ruhusa ya kuekeza   huwa kuna ucheleweshaji wa kufikia lengo lake jamboambalo huwafanya waekezaji kukimbia.
 
Walisema serikali iwetayari kuwafanikishia masuala yao waekezaji kama ilivyo baadhi ya Nchi za Kiafrika (Ruwanda ) ambayo nchi hiyo hivisasa imefanikiwa kwakiasi kikubwa katika uwekezaji jambo ambalo ina ifanya nchi hiyo kupiga hatua kimaendekeo.
 
“Leo ukienda Rwanda kwa suala la uwekezaji ni muda mfupi tu unapatiwa kila kitu, hivyo serikali ya Zanzibar ijifunze kupitia kwao mfanohuo”walisema wajumbe hao.
 
 Hata hivyo wafanya biashara hao walipendekeza kusaidiwa wafanya biashara wadogowadogo wa Zanzibar wakiwemo wafugaji, wavuvi,na wakulima kwani hadi sasa inaonekana watu hao bado wako nyuma katika kuyafikia malengo yao.
 
Mkutano huo wa siku moja ulio beba ujumbe wa uimarishaji wa mazingira ya biashara hapa Zanzibar umejadili masuala mbali mbali ya kibiashara viwanda na uwekezaji pia ulijadili changamaoto zinazo ikabili sekta hiyo hapa Nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>