Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Dkt. Magufuli Acharuka. Ataka Nyumba Wanaokaidi Kuondoka Zizungushiwe Lami.

$
0
0
Na Kunze Mswanyama, DSM
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli,ameiagiza Wakala wa Barabara (Tanroads) kuhakikisha inasimamia sheria kwenye miradi yote ya ujenzi wa barabara licha ya kuwepo baadhi ya wananchi walioishtaki serikali kwani serikali ya CCM ni ya utawala wa sheria.

Waziri Magufuli aliyasema hayo jana alipokuwa akikagua miradi mikubwa ya barabara na madaraja ya jijini Dar es Salaam.

Alitoa amri kwa Tanroads kuhakikisha inajenga barabara katika maeneo yote yaliyomo kwenye mpango bila kuchelea chochote,hata ikibidi kuzizungushia lami nyumba za wale wote watakaokaidi kuvunja nyumba zao kupisha barabara au waliofungua mashauri mahakamani dhidi ya serikali.

Alisema wapo wananchi ambao nyumba zao zimepitiwa na miradi ya barabara wamechukua fedha za fidia na kisha kukimbilia mahakamani kudai fidia hiyo ni ndogo ili kuchelewesha kazi ya ujenzi, na kwamba serikali na itaendelea na ujenzi na nyumba hizo zitazungushiwa lami kwa sababu ni barabara.

Huku akionekana kukasirishwa na kitendo hicho, Magufuli aliasema, “haiwezekani mradi wenye manufaa kwa wananchi wengi ushindwe kukamilika kutokana na wananchi wachache kukaidi maamuzi ya wengi na kukimbilia mahakamani,serikali haitaingilia mahakama,hivyo jengeni barabara hata ikiwezekana muizunguke nyumba hiyo kwa lami ili iwe katikati ya barabara tuone kama mtu huyo ataendelea kuishi hapo,”alisema.

“Naamini kama mkijenga na kuizunguka nyumba hiyo,ipo siku magari yatakosea na kuigonga nyumba na hivyo kutusaidia kumjulisha kuwa eneo hilo ni hatari kwa maisha ya binadamu na ndiyo maana serikali hii sikivu inawalipa ili kupisha miradi hiyo,” alisema.

Akiwa kwenye mradi wa barabara ya mabasi ya mwendo kasi, Dk. Magufuli aliagiza wakala wa mabasi hayo (DART), kuhakikisha hakuna wafanyabishara wadogo wadogo wanaovamia eneo la mradi na kuchelewesha kazi hiyo.

Barabara alizotembelea ni pamoja na ya Tandika-Jet Lumo, Kivukoni-Kimara, daraja la Salenda na la Kigamboni.

Naye Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ambaye pia alikuwepo kwenye ziara hiyo, alisema hakuna mradi utakaosimama au kucheleweshwa kutokana na sababu zozote.

“Nimekuwa nikisikia tu kwamba kuna baadhi ya wananchi wanachelewesha miradi mbalimbali yenye manufaa kwa umma,natoa tahadhari kwa wote wanaofanya hivyo,waache mara moja,miradi hii ina manufaa makubwa kwa Tanzania,” alisema na

“Tutatumia busara zaidi na akili ili kuwaondoa wote wenye tabia hizo lakini ikibidi nguvu itatumika kwani hatuwezi kuacha miradi ya mamilioni ikipotea kwa sababu wananchi wacheche wameamua kutuchelewesha,” alisema.

Awali meneja wa Tanroads Dar es salaam, Mhandisi Julias Ndyamukama,alisema mradi wa mabasi ya mwendo kasi utagharimu shilingi bilioni 288.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>