Na MwandishiMaalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, amesema,ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika operesheni za ulinzi wa Amani umekuwa wa mafanikio makubwa katika urejeshwaji wa hali ya amani na utulivu katika maeneo yenye migogoro.
Hata hivyo amesema pamoja na mafanikio hayo kuna umuhimu wa ushirikiano huo kuboreshwa zaidi na kuwa wenye tija .
Alikuwa akizungumza wakati wa majadiliano ya wazi ya siku moja juu ya ajenda ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, mkazo mkubwa ukielekezwa zaidi katika ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Majadiliano hayo ambayo pamoja na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, pia mshiriki mwingine alikuwa Rais Mstaafu wa Burundi, Pierre Buyoya ambaye ni Mjumbe Maalum wa AU huko Mali na Ukanda wa Sahel. Yameandaliwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa Desemba lipo chini ya Urais wa Jamhuri ya Chad.
Ban Ki Moon ameeleza kuwa kwa miaka mingi ushirikiano kati ya UN na washirika wake wa Kikanda umezidi kuimarika na kwamba Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yamekuwa yakifanya kazi kwa karibu zaidi.
Amesisitiza kuwa ni kutokana na ushirikiano huo, kumekuwapo na uongezeko la uungwaji mkono wa operesheni za kulinda Amani ambazo zimekuwa zikifanyika chini ya Umoja wa Afrika.
Akizungumzia zaidi kuhusu ushirikiano huo na mafanikio yake, Ban Ki Moon amebainisha kwamba, katika Kanda ya Maziwa Makuu, ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika,
Mkutano wa Kimataifa wa Nchi za Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika umesaidia sana katika kurejesha hali ya utulivu katika DRC na eneo la Maziwa Makuu.
Akaeleza pia kuwahuko Somali taasisi hizo mbili kwa maana ya UN na AU pamoja na wadau wengine wanafanyakazi kwa karibu katika kuisaidia serikali ya ya nchi hiyo katika hatua muhimu ya ujenzi wa Amani na ujenzi wa taifa la Somalia.
“Pia tunafanyakazi kwa karibu na AU na Taasisi zingine za Kikanda huko Sudan na Sudani ya Kusini katika suala zima la kutafuta Amani na usalama wa kudumu katika maeneo hayo”. Amesema Katibu Mkuu
Na kusisitiza kuwa pamoja na kuwapo kwa mafanikio bado kuna umuhimu kwa kuongeza juhudi zaidi katika eneo hilo la ushirikiano na hasa kutokana na ukweli kuwa walinzi wa Amani wanaohudumia katika Taasisi hizo wanakabiliwa na changa moto nyingi na hatari kubwa zaidi.
Ban Ki Moon, ameleza kuwa walinzi hao wa Amani wanafanyakazi katika mazingira magumu na hatarishi huku wakilazimika kukabiliana na makundi ya waasi wenye silaha, makundi ya kigaid i na makundi ya uhalifu wa kupangwa.
Na kwa sababu hiyo anasema ili kuboresha ushirikiano uliopo baina ya UN na AU panahitajika mbinu na fikra mpya na mbadala zitakazokwenda sambamba na mabaliliko yaliojitokeza hivi sasa katika eneo hilo la operesheni za ulinzi wa Amani.
Aidha anasema panahitajika ushirikiano wa kisiasa bali pia uwepo wa uwazi, uwajibikaji na vile vile kujua nani anafanya nini wapi na kwa wakati gani na majukumu ya kila Taasisi.
Akasisitiza kuwa Jumuiya ya Kimataifa inatambua vema kuwa migogoro inayoikumba si matatizo ya Afrika peke yake bali inahusu Jumuiya yote ya Kimataifa na kwamba utatuzi wake unahitaji ushirikiano wa pamoja na kufanya kama kitu kimoja.
Akizungumzia kuhusu Afrika kuwa na vyanzo vyake vya mapato vitakavyogharamia shughuli za ulinzi, Ban Ki Moon amesema inagawa na yamekuwa muumini wa dhana hiyo lakini bado anaamini kuwa mchango wa Jumuiya ya Kimataifa unahitajika pia.
AkaushukuruUmojawaAfrikakwanamnaambavyoimekuwaikishughulikiamigogorombalimbaliinayojitokezakatikaAfrikapamojanaushirikiano wake naUmojawa Mataifa