Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Zaidi ya 1bn/- zapelekwa kaya maskini

$
0
0
Na Asya Hassan
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF-3) upande wa Zanzibar umetumia shilingi 1,056,819,637 kuziwezesha kaya masikini,ambapo shehia 40 za Unguja na Pemba zimefaidika na fedha hizo.

Kwa Unguja shilingi 401,477,884  zimetolewa kwa awamu sita kuanzia Januari hadi Disemba na Pemba zimetolewa shilingi 655,341,753 kwa kwa awamu tano kuanzia Januari hadi Septemba.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Migombani, Mratibu wa mradi huo Unguja, Fatma Mohammed Juma, alisema kwa upande wa Pemba mgao wa mwezi wa Disemba bado hawajaupata.

“Mpaka hivi sasa mpango huu wa ruzuku ya kuziwezesha kaya masikini imeshatolewa kwa awamu sita ambapo Januari zimetolewa shilingi 70.448 milioni,Machi 83.45 milioni,Mei 76 milioni,Julai 67.92 milioni , Septemba 78.11 milioni na Disemba shilingi 86.73 milioni,” alisema.


Alisema kwa upande wa Pemba Januari ziligawiwa shilingi 123 milioni, Machi 136.272 milioni, Mei 136.34 milioni, Julai 123.4 milioni na Septemba 136 milioni na mwezi wa Disemba bado hatujapata idadi yake,” alisema.

Alisema kaya 6,855 zinahusika na mpango huo ambapo Unguja kuna kaya 2,674 na Pemba kaya 4,181.

Mratibu huyo alisema bajeti ya malipo kwa awamu hizo ni shilingi 1,042,217,465 ambapo Unguja ni shilingi 489,669,633 na Pemba ni shilingi 552,547,832.

Alisema fedha hizo hutolewa kwa mashariti maalum ikiwemo kuwasomesha watoto,kuwapeleka hospitali watoto pamoja na mama wajawazito.

“Tokea kuwepo kwa mpango huu wa kuziwezesha kaya masikini kwa kiasi fulani jamii imefanikiwa kwani wapo watoto waliokuwa hawaendi skuli wamerudi skuli na wanaohitaji kwenda hospitali wanapelekwa, kwa kweli mpango huu unasaidia kwa hatua kubwa katika kupunguza umasikini kwa kaya hizi masikini,”alisema.


Alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi ambao wananufaika na mpango huo kuutumia kama inavyotakiwa ili kuweza kujikwamua na ukali wa maisha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>