Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Hyria Ally (miezi 9) Kutoka Zanzibar, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Zulekha Said. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Yahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Amina Yahya. Picha na OMR
Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo. Picha na OMR
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, waakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR
Baadhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo. Picha na OMR