Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wanaoishi na VVU Hawajatambuliwa Rasimu ya Katiba Mpya.

$
0
0
Na Khamisuu Abdallah
WATU wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar wameiomba Tume ya marekebisho ya katiba kuvifanyia marekebisho baadhi ya vifungu na vyengine kuviongeza ili kuifanyia mamuzi sahihi katiba mpya hasa kwa watu wenye kuishi na virusi vya Ukimwi.

Wakitoa maoni yao katika mkutano wa kuchangia katiba hiyo ulioshirikisha Wilaya sita za Zanzibar kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ulioandaliwa na ZAPHA+ ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar, washiriki hao walisema vipengele vingi vya katiba hiyo havikuwapa fursa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kushiriki mambo mbalimbali ya msingi.

Aidha walisema katika katiba hiyo vipengele vingi vimepungua kutokana na vifungu hivyo kutoonesha haki na fursa za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kama ivyoainishwa kwa watu wenye ulemavu.

Walisema kuwa watu wanaoishi na VVU wamekuwa wakikosa haki zao za msingi kutokana na kunyanyapaliwa na kuonekana hawana umuhimu hasa katika fursa ya ajira na kupata utambulisho wa kwenda nje ya nchi.

"Kiukweli sisi tunakosa haki zetu nyingi kutokana na maradhi haya pindi tukienda kuomba ajira kwanza hupimwa vvu na tukionekana tu mtu anakosa ajira na hata kwa wale waliokuwa makazini huwa wanafukuzwa usiseme tukipata fursa ya kwenda nje ya nchi huwa tunakataliwa katakata na kunyanyapaliwa" walieleza washiriki hao.

Washiriki hao walisema kuwa rasimu hiyo haijaweka wazi makundi madogo madogo hivyo wameiomba tume hiyo kuviainisha vifungu hivyo ili na watu wenye kuishi na virusi vya ukimwi wawekwe kwenye makundi ili kuweza kupata haki zao za msingi.

"Rasimu hii tumeiona hapa imeonesha makundi madogo madogo lakini haikuainisha makundi haya ni yapi, hivyo tunaiomba tume kuainisha makundi hayo ili na sisi watu wenye virusi vya Ukimwi tuainishwe na tuweze kupata haki zetu za msingi" walisema washiriki hao.

Hata hivyo walifahamisha kuwa katika rasimu hiyo haikuweka hata kipengele kimoja kinachoonesha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kuwa wana haki ya kuingia katika Baraza la Wawakilishi.

Wakizungumzia suala la watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi kuendelea kunyanyapaliwa wajumbe hao wameiomba tume hiyo kuainisha kifungu kitakachoonesha mabaraza ya watoto hasa kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi ili jamii iweze kuacha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwanyooshea vidole watoto hao.

Wakizungumzia kipengele cha kuwepo kwa serikali tatu katika rasimu hiyo washiriki hao walisema ili kuudumisha na kuenzi muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni vyema kuwepo kwa serikali mbili kwani kuwepo kwa serikali tatu umasikini utazidi hapa nchini.

Hivyo washiriki hao wameiomba tume hiyo kuangalia watu wanoishi na virusi vya ukimwi ili waonekane na wao wana haki katika jamii kama watu wengine.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya ZAPHA+, Hasina Hamad, akifungua mkutano huo aliwataka washiriki hao kuichangia rasimu hiyo kwa umakini zaidi ili iweze kuleta maslahi ya taifa na sio kwa mtu binafsi.

Pia aliwanasihi washiriki hao kuitumia fursa hiyo kutoa maoni yao juu ya katiba wanayoitaka kwa wao na hata kwa vizazi vijavyo.

Mkutano huo wa siku mbili uliandaliwa na Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar
ZAPHA+

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>