Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35049

Watanzania waaswa kutunza amani

$
0
0
Na Mwanajuma Abdi, DAR ES SALAA
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa, Mchungaji wa kanisa la Tanzania Fellowship, Godfrey Malassy, amesema amani ya Tanzania ipo kama ‘yai’, ambalo likivunjia haliwezi kurudishwa tena, hivyo aliwahusia baadhi ya wanasiasa kuacha kutumia lugha za uchochezi, za kuvuruga na kuhataraisha utulivu nchini.

Hayo aliyasema jana, wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa habari Maelezo, kuelezea dua maalum ya kitaifa itakayofanyika mkesha wa maka mpya Disemba 31, ambayo itahusisha mikoa 16 ya Tanzania, ambapo kwa Dar es Salaam itafanyika uwanja wa taifa na Zanzibar utafanyika uwanja wa Amaan.

Alisema amani ya Tanzania imebarikiwa na Mwenyezi Mungu, hivyo wanasiasa na wananchi wanatakiwa kuienzi, kuidumisha na kuilinda badala ya kutoa lugha za umwagaji damu ambazo zinaweza kuliingiza taifa katika matatizo makubwa.

Kauli mbiu katika mkesha huo ni ‘itunze, ilinde,ihubiri amani ya nchi yako’, ambapo alitoa wito kwa Watanzania kutochezea amani kwani ikipotea hawataweza kuirejesha tena, hivyo kuna kila sababu ya kuliinda.


Alisema mkesha huo umewashirikisha waimbaji wa kwaya kutoka madhehebu mbali mbali ili nchi iweze kuombewa amani kwa kumaliza mwaka kwa usalama na kuukaribisha mwaka mpya.

Alisema  kuombea dua taifa haihusishi dini fulani hivyo alitoa wito kwa waumini wa dini nyengine kuungana nao pamoja katika kuliombea taifa.

Akitoa mfano wa Zanzibar kuna Waislamu zaidi ya asilimia 99 lakini mkesha huo unafanyika katika uwanja wa Amaan, ambapo wakaazi wa huko wameipokea vizuri dua hiyo, hivyo kuna kila sababu ya watu kuungana na kushirikiana ili kuombea nchi.


Alisema baadhi ya nchi za Afrika zinalia kila siku kutokana na kukosekana amani, wanashindwa kulima vizuri pamoja na shughuli za kimaendeleo akitoa mfano nchi ya Congo na kwengineko ambako utulivu umekosekana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35049

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>