Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Vyama vya Siasa Vyaombwa Kuchangia Kufanikisha Miaka 50 ya Mapinduzi.

$
0
0


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud amesema sherehe za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zina lengo la kuendeleza azma ya Mapinduzi matukufu ili kufikia shabaha na kuonesha mabadiliko na maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi hicho.

Waziri Aboud aliyasema hayo jana ofisini kwake Vuga wakati akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa kuhusu ushiriki wao katika kuadhimisha sherehe hizo.

Alisema serikali imeamua kuvishirikisha vyama vya siasa ili kuepusha malalamiko miongoni mwa vyama.

Alisema sherehe za kutimiza miaka 50 Mapinduzi ya Zanzibar ni za kitaifa na kuvitaka vyama hivyo kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo ili kudumisha amani na umoja wa kitaifa uliopo nchini.

Akizungumzia changamoto zinazozikabili sherehe hizo, alisema uhaba wa fedha huzorotesha maandalizi ya sherehe hizo, hivyo alivitaka vyama vya siasa kushirikiana na serikali katika kuzifanikisha.

Akizungumzia suala la sare zitakazovaliwa katika kuadhimisha sherehe hizo, alivitaka vyama vya siasa kutumia rangi za bendera ya nchi ili kuondosha mvutano baina ya wafuasi wa vyama hivyo pamoja na kudumisha umoja wa kitaifa.

“Hatukatazi mtu kuvaa sare ya chama chake, bali kuvaa sare zenye rangi ya bendera ni uamuzi wa serikali ili kuondosha mvutano usiokuwa na haja,” alibainisha.

Aliongeza kuwa kutokana na uhaba wa fedha katika kugharamia fulana kwa wananchi wote, aliyaomba mashirika na kampuni binafsi kulichukulia suala hilo kuwa la wote, sambamba na kuzingatia rangi kulingana na bendera ya nchi bila ya kuhusisha rangi ya chama.

Aidha alisema matangazo yanayotolewa katika sherehe hizo hayalengi chama kimoja bali kwa vyama vyote kwa lengo la kuwafikia wananchi wote.

Hata hivyo aliongeza kuwa sherehe hizo zinakwenda sambamba na uwekaji wa mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wa vyama vya siasa nchini waliishukuru serikali kwa kukubaliana na wazo la kutovaa sare za vyama vyao na badala yake kutumia rangi za bendera ya serikali.

Aidha waliwataka wafuasi wa vyama vyao kushirikiana na serikali katika kuadhimisha sherehe hizo kwa kudumisha umoja na mshikamano wakitaifa uliopo ili kuepusha mizozano ya kisiasa.

Sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatarajiwa kufikia kilele chake Januari 12, 2014.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>