Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Maambukizi ya VVU kwa Wanaoishiriki Mapenzi ya Jinsia Moja Yapungua

$
0
0
Kauthar Abdalla na Asya Hassan
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema maambukizo ya Virusi vya Ukimwi kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja yamepungua kutoka asilimia 12.3 (2007) hadi asilimia 2.6 (2012).

Maambukizi ya ugonjwa huo watumiaji wa dawa za kulevya kwa njia ya sindano yamepungua kutoa asilimia 16 (2007) hadi asilimia 11.3 mwaka uliopita.

Aidha akinamama wajawazito wameanza kujifungua bure katika hospitali za serikali na hivyo kupunguza vifo vya watoto.

Waziri wa Afya, Juma Duni Haji alisema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2013-2014 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi.

Waziri Duni alisema katika kufikia malengo ya milennia katika bara la Afrika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejidhatiti kupambana na tatizo la afya na vifo vya akinamama ambapo wanatakiwa kujifungua katika vituo vya afya.

Alisema katika kuweka kipaumbele hicho vifo vya akinamama kwa sasa vimedhibitiwa na kupungua kwa kiwango kikubwa.

Alisema jumla ya akinamama wajawazito 9,176 walifika katika hospitali za serikali kwa ajili ya kujifungua ambapo akinamama 7,732 walipatiwa huduma hiyo huku 522 wakijifungua kwa njia ya upasuaji na 20 walifariki dunia.

Duni alisema miongoni mwa tatizo kubwa ambalo limekuwa chanzo cha vifo vya akinamama ni pamoja na kifafa cha mimba na upungufu wa damu.

Alisema akinamama wajawazito wameanza kupokea wito wa serikali wa kujifungua katika hospitali za serikali ambapo kwa kiasi kikubwa tatizo la vifo vya akinamama limepungua kwa kiwango kikubwa.

Aidha alisema huduma za uzazi kwa akinamama wanaofika katika hospitali za serikali ni bure kwa mujibu wa agizo la Rais wa Zanzibar.

Aidha alisema malengo makuu ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2013-2014 ni kuanzishwa kwa chanjo mpya ya maradhi ya kuharisha pamoja na uti wa mgongo.

Alisema Wizara pia imeanza mkakati wa kupambana na maradhi ya matende pamoja na kichocho ambayo yamekuwa yakiwasumbuwa watoto kwa kiwango kikubwa.

Duni alisema katika kupambana na maradhi ya kichocho jumla ya wanafunzi 48 wa skuli walifanyiwa uchunguzi na wengine kupatiwa dawa.

Alisema juhudi za ujenzi wa bohari kuu ya dawa kwa sasa zipo katika hatua nzuri ambapo itahakikisha suala zima la upatikanaji wa dawa na uhifadhi wake katika kiwango cha kitaalamu zaidi.

Alisema miongoni mwa majukumu makubwa ya Wizara ya Afya ni kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa na kuwasafirisha nje ya nchi baada ya kushindikana matibabu yao.

Alisema katika mwaka 2012-2013 , wagonjwa 223 waliorodheshwa na bodi kwa ajili ya kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

Aidha alisema wagonjwa 1,445 walisafirishwa nje ya nchi na wagonjwa 45 walipelekwa Tanzania Bara kwa matibabu zaidi huku serikali ikitumia shilingi milioni 920.

Waziri Duni aliyapongeza mashirika ya kimataifa ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), Mfuko wa Global Fund na Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) kwa juhudi zao za kusaidia maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo kupambana na maradhi sugu ya kifua kikuu pamoja na ukoma.

Wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 21,318,000,000 kwa kazi za kawaida, ruzuku, mishahara na maposho.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hassan Hamad Omar alisema kutokana na umuhimu wa huduma za afya na dawa kamati inashauri Wizara kutafuta kampuni nyengine ya kuagiza na kuingiza dawa nchini badala ya kutegemea bohari kuu ya dawa ya Dar es Salaam pekee ambayo nao huchangia uhaba wa upatikanaji wa dawa katika hospitali na vituo vya afya katika muda unaotakiwa.

Hata hivyo, alisema kitengo cha kupambana na magonjwa yasio ya kuambukiza kinaendelea kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na magonjwa hayo na kamati inasisitiza wizara, pamoja na kuwepo kwa kitengo kuendelea kusimamia muongozo wa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza ili uweze kukamilika na kuanza kutumika.

Alisema kumekuwa na wananchi ambao hushindwa kuhudhuria hospitali na vituo vya afya kutokana na kushindwa kumudu gharama za afya hivyo kamati imesema ina matumaini makubwa kwamba kuanzishwa kwa bima ya afya kutawawezesha wananchi wanyonge kufaidika na huduma za afya kwa kadri watakavyozihitaji.

N ae Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub akichangia bajeti hiyo alisema utatibu wa kuifanya hospitali ya Mnazimmoja kuwa ya rufaa ni mzuri kwani utapunguza msongamano wa watu lakini vifaa vya kutumika havipo na huduma haipatikani.

Aidha alisema wanafunzi kufanya mazoezi moja kwa moja katika miili ya watu bila ya kuwepo muangalizi wa uhakika ni tatizo ambalo linahitaji umakini.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>