Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tazara Waagizwa Kurejea Kazini Jumatatu.

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amewaagiza wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Reli (TAZARA) wanaoendelea na mgomo, kurejea kazini Jumatatu.

Dk. Mwakyembe alisema bungeni jana, mgomo unaofanywa na wafanyakazi hao upo nje ya utaratibu wa kisheria kwa sababu hakukuwa na mazungumzo kati ya menejimenti ya TAZARA na chama cha wafanyakazi wa reli.

Wafanyakazi hao wanagoma wakitaka walipwe mishahara yao ya kuanzia mwezi Mei hadi Agosti.

Hata hivyo, Waziri Mwakyembe alisema TAZARA imeanza kulipa mishahara ya wafanyakazi wake ya mwezi Mei kwa upande wa Tanzania na Zambia.

Aidha alisema mishahara ya mwezi Juni, Julai na Agosti iko tayari na itaanza kulipwa kuanzia Jumatatu.

Alisema mishahara hiyo tayari imeshapelekwa benki kwa hatua za malipo na kilichobakia ni benki kuiingiza kwenye akaunti za wafanyakazi hao.

Alisema mgomo huo umeleta athari kubwa, ambapo wakaazi 46,000 wa Dar es Salaam wameathirika kwa kukosa huduma za reli tokea mgomo huo uanze.

Alisema abiria wengine 24,000 wenye tiketi wakiwemo watalii walishindwa kusafiri na kusababisha Mamlaka kuwarejeshea fedha zao.

Alisema hali ya mapato katika mamlaka hiyo sio nzuri na kwamba katika kipindi cha mwezi uliopita Mamlaka ilijiendesha kwa hasara.

Aliiagiza TAZARA kufuatilia madeni inayowadai wateja wake wakubwa na kuhakikisha yanalipwa haraka iwezekanavyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>