Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mikakati na mipango ya Miaka 5 ijayo ya Sauti za Busara”

$
0
0
 
16 Septemba 2013
 
Busara Promotions ni Taasisi inayoandaa tamasha la muziki la Sauti za Busara, ikishirikiana na bodi ya wadhamini, uongozi, wafanyakazi pamoja na wageni kutoka sekta ya sanaa na utamaduni Tanzania waliokutana mwishoni mwa wiki kupanga mikakati na mipango katika hoteli ya Bluebay Beach Resort iliyopo Kiwengwa, Zanzibar ili kupitia mafanikio ya muongozo uliopita na kupanga mikakati na shughuli ya miaka mitano ijayo.
 
Imedhaminiwa na mfuko wa Kiholanzi Hivos, Bluebay Beach Resort Zanzibar na wawezeshaji kutoka PEN Kenya, timu nzima ya Busara Promotions ilijumuika pamoja ili kuweza  kupanga mwongozo mpya katika taasisi, ambayo imejenga ubora na nguvu katika kutangaza utamaduni na muziki wa Afrika Mashariki na kati, kitaifa na kimataifa kwa miaka kumi iliyopita.
 
Ingawa Taasisi inajulikana kwa uandaaji wa tamasha la muziki ambalo hufanyika moja kwa mwaka lijulikanalo kwa jina la Sauti za Busara (Sounds of Wisdom), Busara Promotions pia huhusika  nyuma ya pazia katika sekta ya muziki, kujenga thamani ya muziki duniani kote na kanda zote kwa ujumla, kujenga ujuzi na kuwapatia nafasi wasanii na wanamuziki, wataalam wa muziki,kuimarisha miundombinu na kujenga mitandao ya kikanda na kitaifa.
 
Mipango ya miaka mitano ijayo ni kujenga mafanikio ya awali ya Busara Promotions pamoja na kutambulisha mawazo mapya na miradi ikiwa ni pamoja na kuongeza shoo zaidi za utamaduni kwa Taasisi kwa mwaka mzima.
 

Busara Promotions inatarajia kuwa hai katika mashirikiano na wasanii na wataalam wa muziki na kazi, mafunzo na nafasi katika mitandao pamoja na kuimalisha muonekano wa muziki wa Kiafrika na maelezo katika mitandao.
 
Busara Promotions inapenda kutangaza kuwa wakati wa majadiliano, Bodi ya wadhamini imechagua wanachama wapya watatu kujiunga na bodi ya wadhanimi ambao ni: Ally Saleh, Mzanzibari ni mwandishi wa habari anaejulikana, aliwahi kufanya kazi na Busara Promotions wakati wa Kongamano la Viongozi wa Utamaduni na ukuaji wa uchumi Zanzibar mwaka 2011 Novemba. Aliongoza majadiliano hayo kwa wadau wa biashara, utalii na wadau wengine wanaohusika katika taasisi za utamaduni katika kuleta faida kwa wazawa.
 
Julia Bishop, ni mshauri mtaalam na mkurugenzi mwanzilishi wa Chama cha Wawekezeji sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI), kuleta kwake utaalam wake katika utalii na biashara katika bodi ya wadhamini Busara Promotions. Verena Knippel amesaidia baadhi ya watanzania katika ratiba ya TV na filamu. Amewahi kuishi na kufanya kazi Zanzibar kwa muda wa miaka mingi baada ya hapo alihamia Dar es Salaam na kujiunga na DFID kama mtaalam wa kusaidia bajeti. Wanachama hawa watatu wa bodi ya wadhamini watasaidia kuiongoza Busara Promotions na kutimiza malengo ya miaka ijayo, kwa kuchangia ujuzi wao mbali mbali na uzoefu wao katika timu.
 
Kwa wakati huo huo, Bodi ya wadhamini wawili ambao ni waanzilishi, Hilda Kiel na Emerson Skeens, wamejiuzulu katika nafasi zao kama bodi ya wadhamini na kuwa wanachama washauri wa Busara. Mwenyekiti wa Bodi, Simai Mohammed Said, aliwashukuru kwa huduma zao za miaka mingi katika taasisi na kuwapongeza kwa kuendelea kushiriki kuwa washauri.
 
Busara Promotions inaandaa toleo la 11 la tamasha la muziki la Sauti za Busara, litakalo fanyika kuanzia tarehe 13 mpaka16 February 2014, Mji Mkongwe, Zanzibar. Tamasha litashirikisha majina bora ya wasanii wa muziki wa Kiafrika.
 
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi mtendaji wa Busara Promotions, Rebecca Corey, kupitia barua pepe ifuatayo: rebecca@busara.or.tz.
 
Shukrani za dhati kwa Bluebay Beach Resort, Zanzibar na wadhamini wetu wa  Sauti za Busara 2014: Royal Norwegian Embassy, Hivos, Goethe Institute, Memories of Zanzibar, Azam Marine, Ultimate Security, Zanzibar Unique Ltd., SMOLE II na wahisani wetu wote

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>